IQNA

Ibada ya Umrah

Waislamu 100 waliosilimu karibuni washiriki Umrah

12:12 - December 29, 2022
Habari ID: 3476323
TEHRAN (IQNA) – Katika mpango uliobuniwa na mamlaka ya Saudia, Waislamu wapya 100 walitembelea Msikiti Mtakatifu wa Makka na Msikiti wa Mtume SAW mjini kutekeleza ibada ya Hija ndogo ya Umrah kwa mara ya kwanza.

Ofisi ya Urais Mkuu wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitukufu iliwapokea Waislamu hao katika fremu ya Mpango wa Hija wa Dunia wa waliosilimu ambao mwaka huu ni kutoka nchi 30.

Mpango huo ni pamoja na kuwafahamisha Waislamu wapya misingi ya Uislamu na pia kuwafundisha kuhusu Umra .

Kwa mujibu wa mpango uliopo, mutawwif (waelekezi wa Mahujaji) Huandamana na Waislamu wapya ndani ya Msikiti Mkuu na pia wamewatembeza Kituo cha Mfalme Abdulaziz cha Kushona Kiswa ya Kaaba Tukufu.

Aidha Waislamu hao wapya walipokelewa Madina na kutembelea Msikiti wa Mtume SAW.

 

3481860

captcha