IQNA

Ibada ya Umrah

Kibali Rasmi cha Umrah kinahitajika kwa watoto walio na umri wa zaidi ya miaka 5

21:40 - December 11, 2022
Habari ID: 3476232
TEHRAN (IQNA) – Wakuu wa Saudi Arabia wametangaza kwamba umri wa chini kabisa wa kutoa kibali rasmi cha Umrah ni miaka mitano.

Mamilioni ya Waislamu, ambao hawawezi kumudu ibada ya kwa sababu mbali mbali, kila mwaka humiminika Saudi Arabia kwa ajiliya Hija Ndogo au Umrah katika Msikiti Mtakatifu wa Makka.

Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi ilibainisha kwamba umri wa chini unaoruhusiwa kufanya Umra ni miaka mitano, lakini ilisema watoto wanapaswa kuandamana na wazazi katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, Al Masjid al Haram, ambao ndani yako imo Kaaba Tukufu.

"Umri wa chini wa kupata kibali cha umrah ni miaka mitano, mradi mtoto hajaambukizwa corona," wizara hiyo ilisema

Saudi Arabia hivi majuzi ilizindua jukwaa la kielektroniki, lililoundwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za umrah ikiwa ni pamoja na kutembelea miji mitakatifu ya Makka na Madina.

Jukwaa la nusuk.sa linawawezesha Waislamu wanaotaka kushiriki katika ibada ya Umrah au kutembelea maeneo matakatifu kupata visa na vibali vinavyohitajika.

Katika hatua mpya ya kuwezesha, Saudi Arabia ilisema mapema mwezi huu kwamba raia wake wanaweza kutuma maombi ya kuwaalika marafiki zao nje ya nchi kutembelea ufalme huo na kutekeleza ibada ya umrah.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia ilisema raia wanaweza kutuma maombi ya visa ya ziara ya kibinafsi kupitia jukwaa lake la e-visa, na kumruhusu mwenye visa hiyo kutekeleza ibada ya Umrah na kuzunguka ufalme huo ikiwa ni pamoja na maeneo ya kidini na ya kihistoria.

3481622

captcha