IQNA

Umrah

Wakaazi wa Makka wahimizwa kuwatanguliza Mahujaji wa Kigeni katika Msikiti Mkuu

15:16 - March 22, 2024
Habari ID: 3478555
IQNA - Wakaazi wa mji mtakatifu wa Makka nchini Saudia wamehimizwa kutoa kipaumbele kwa Mahujaji wa kigeni katika Masjid al-Haram au Msikiti Mkuu.

Wakuu wa Saudia wametoa wito huo huku mji huo mtakatifu ukishuhudia wimbi la waumini katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika mwezi huu uliobarikiwa, Waislamu kutoka ndani na nje ya Saudi Arabia wamekuwa wakielekea kwa wingi kwenye Masjid al-Haram kutekeleza Umra au Hija ndogo, na kuswali.

“Wageni wa Mwenyezi Mungu ni wageni wa watu wa Makka. Kwa hivyo, tuwe wakarimu na tuwape nafasi kwenye Msikiti Mkuu, "Wizara ya Hajj na Umrah ya Saudi ilisema kwenye akaunti yake ya X, zamani Twitter.

Wizara hiyo ilitoa wito kwa wakaazi wa Makka kupunguza msongamano kwa kuswali katika misikiti mingine ya jiji hilo, ikisema kuwa mji wa  Makka kwa ujumla ni haram au sehemu takatifu.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kawaida huashiria msimu wa kilele wa Umrah.

Katika miezi ya hivi karibuni, suhula nyingi zimezinduliwa kwa Waislamu wa ng'ambo kuja nchini kufanya Umra.

Waislamu walio na aina tofauti za visa vya kuingia kama vile visa binafsi, ziara na utalii wanaruhusiwa kufanya Umra na kutembelea Al Rawda Al Sharifa, lilipo kaburi la Mtume Muhammad (SAW) katika Msikiti wa Mtume Madina baada ya kuweka miadi ya kielektroniki.

Mamlaka ya Saudia imeongeza muda wa visa ya Umrah kutoka siku 30 hadi 90, na kuruhusu wamiliki wa visa hiyo kuingia katika ufalme huo kupitia njia zote za ardhini, anga na baharini na kuondoka kutoka uwanja wowote wa ndege. Mahujaji wanawake hawatakiwi tena kusindikizwa na walezi wa kiume.

3487687

Habari zinazohusiana
captcha