Haya ni kwa mujibu wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon, ambalo, katika taarifa, lilitoa salamu za rambirambi kutokana na kifo cha msomi huyo wa Kiislamu.
Mkutano huo ulimtaja kuwa mwenezaji na mhubiri wa Uislamu wa kweli ambaye alitaka kukuza umoja wa Waislamu na kukabiliana na mikondo potofu.
Aliwafundisha vijana wengi wa Kiislamu kuwa wahubiri na viongozi, taarifa hiyo ilisema.
Aidha wanazuoni hao wamemtaja Marhum Hilbawi kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kutoa uungaji mkono kwa Mapinduzi ya Kiislamu baada ya ushindi wake mwaka 1979.
Pia aliunga mkono na kutetea muqawama au mapambano ya Palestina na Lebanon dhidi ya Israel kwa nguvu zake zote, ilisema taarifa hiyo.
Halikadhalika taarifa hiyo imeashiria namna mwanazuoni huyo alivyoshambuliwa na maadui kwa uthabiti wake wa kushikamana na kanuni za kimsingi katika fikra za Kiislamu na kusema mashambulizi hayo hayakuathiri misimamo yake.
Hilbawi alifariki mjini London siku ya Jumatano na kuzikwa katika makaburi katika mji mkuu wa Uingereza.
Alizaliwa mwaka wa 1939, Hilbawi aliwahi kuwa msemaji wa Harakati ya Ikwanul Muslimi ( Muslim Brotherhood) katika nchi za Magharibi lakini baadaye akaliacha kundi hilo.
Hilbawy anajulikana kwa maandishi na maoni yake kuhusu Uislamu, uchambuzi wa kisiasa na ulimwengu wa Magharibi.
Pia alipata umaarufu kwa harakati za Kiislamu barani Ulaya na kusaidia katika kuanzisha mashirika kadhaa ya Kiislamu, pamoja na Jumuiya ya Waislamu wa Uingereza mnamo 1997.
4125784