IQNA

Wanamichezo Waislamu

Mchezaji chipukizi wa Manchester United awavutia wengi akisoma Qu'ran Tukufu huko Trafford

18:20 - March 16, 2023
Habari ID: 3476715
TEHRAN (IQNA)- Mchezaji chipukizi wa akademia ya Soka ya klabu maarufu ya Manchester United nchini Uingereza amewavutia wengi baada ya klipu yake akiwa anasema Qur'ani Tukufu kuenea mitandaoni. Katika kilipu iliyosambazwa na kaka yake, Amir Ibragimov mwenye umri wa miaka 15 anaonekana akisoma sehemu ya Surah Al-Furqan ndani ya Kituo cha Trafford mjini Manchester nchini Uingereza

Video imevutia zaidi ya watu 6K kwenye Instagram katika kipindi cha muda mfupi na imesambazwa kwenye majukwaa mengi ya mitandao ya kijamii. Wengi wamempongeza Amir kwa usomaji wake mzuri wa Qur'ani Tukufu.

Mwaka jana Amir aligonga vichwa vya habari aliposaini mkataba mpya na Manchester United. Mwanasoka huyo mwenye sifa nyingi alitia saini mkataba ambao utamfanya abaki katika klabu hiyo katika kipindi chote cha udhamini wake hadi atakapotimiza umri wa miaka 17.

Kijana huyo ni mmoja wa wachezaji bora katika Akademia ya Soka ya Manchester United na alikuwa nahodha wa timu ya umri wa chini ya miaka 14 waliposhinda Kombe la Albert Phelan dhidi ya Man City. Mzaliwa wa Russia, Amir anatoka katika familia yenye vipaji na kaka yake mkubwa Ibragim, 18, ni mpiganaji wa MMA huku kaka yake mwingine akiwa katika Akademia ya Manchester  United akichezea timu ya chini ya umri wa miaka 12.

Hii hapa chini klipu yake akisoma Qur'ani Tukufu.

4128342

captcha