IQNA

Wito wa kususia shirika la Puma ambalo linafadhili ligi ya Israel

14:41 - September 24, 2021
Habari ID: 3474334
TEHRAN (IQNA)- Maandamano yanafanyika maeneo mbali mbali duniani kulitaka shirika la Ujerumani la mavazi la michezo la Puma kusitisha uungaji mkono kwa utawala wa kibaguzi wa Israel.

Waandamanaji hivi karibuni walijumuika nje ya makao makuu ya Puma huko Manchester, Uingereza ambao wamelitaka shirika hilo lisitisha uhusiano wao na ligi ya soka ya utawala wa Israel ambao msingi wake ni ubaguzi wa rangi.

Katika siku za hivi karibuni pia mitandao ya kijamii imeshuhudia kupanda chati hashtegi ya #BoycottPuma, yaani ‘susia puma ili kulishinikiza shirika hilo kusitisha uungaji mkono wake kwa utawala dhalimu wa Israel ambao unakalia kwa mabavu na kuzikoloni ardhi za Palestina sambamba na kuwakandamiza kinyama Wapalestina wanaopigania uhuru wao.

Harakati ya Kimatiafa ya Kususia Israel, BDS, ambayo inaongoza kampeni hiyo imesema Puma imehusika katika ukiukwaji wa sheria kimataifa na haki za binaadamu kwa sababu ni mfadhili mkuu wa Shirikisho la Soka la Israel ambalo linajumuisha timu ambazo ziko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kinyume cha sheria. Aidha zaidi ya timu 200 za Palestina  pia zimeitaka Puma kusitisha ufadhili na uungaji mkono wa Shirikisho la Soka la Israel.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2018 Shirika la Adidas lilisitisha ufadhili wake kwa timu ya taifa ya utawala haramu wa Israel kufuatia mashinikizo.

3998886

Kishikizo: bds ، puma ، palestina ، israel
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha