IQNA

Mwanamichezo Muislamu

Wachezaji wa MAN U waunga mkono mchezaji Muislamu aliyekataa vazi la ufuska

11:34 - December 05, 2024
Habari ID: 3479860
IQNA-Wachezaji wa Manchester United, moja ya timu kubwa katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) waliamua kutovaa vazi la Adidas linalounga mkono ufuska wa watu wenye uhusiano wa jinsia moja wakati wa mechi dhidi ya Everton Jumapili iliyopita, ikiwa ni hatua ya kumuunga mkono mchezaji mwenzao Muislamu, Noussair Mazraoui, ambaye alikuwa wa kwanza kukataa kufanya hivyo.

 

Mwanasoka huyo wa Morocco alieleza kuwa uamuzi wake ulitokana na imani yake ya Kiislamu, ndiyo maana alikataa kushiriki katika kampeni ya "Rainbow Laces" inayokuzwa na chapa ya Ujerumani, inayolenga kuangazia kile kinacho daiwa eti ni "usawa na kujumuishwa" kwenye EPL. Ukweli ni kuwa ni kampeni chafu ya kuhimiza uhusiano wa watu wa jinsia moja.

Wenzake waliamua kumuunga mkono na pia walijizuia kuvaa koti la Adidas. Manchester United ilitoa taarifa kufafanua msimamo wao juu ya kampeni huku ikisisitiza haki ya wachezaji kutoa maoni yao: "Wachezaji wana haki ya kutoa maoni yao, hasa kuhusu imani yao, na maoni haya wakati mwingine yanaweza kutofautiana na yale ya klabu."

Msimamo wa Mazraoui unaonyesha maadili ya kitamaduni na kidini. Vitendo vya ushoga na usagaji pamoja na ufuska wowote ule husika ni marufuku kabisa katika Uislamu.

Qur'ani Tukufu inalaani vitendo vya ushoga waziwazi na kuvitaja kuwa ni dhambi. 

4252281

captcha