IQNA

Pogba wa Man U aunga mkono wanawake Waislamu India wanaokandamizwa kwa kuvaa Hijabu

21:31 - February 10, 2022
Habari ID: 3474914
TEHRAN (IQNA)- Mchezaji nyota wa Manchester United, Paul Pogba aliingia kwenye mitandao ya kijamii siku ya Alhamisi na kusambaza video yenye kuwatetea wanawake Waislamu India wanaovaa Hijabu kufuatia mzozo unaoendelea kuhusu Hijab katika Jimbo la Karnataka nchini India.

Wanafunzi wa kike wa Kiislamu huko Karnataka wanapinga kupigwa marufuku kwa hijabu vyuoni.

Pogba ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa ni Muislamu mcha Mungu  na alisambaza video kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram ambapo klipu hiyo ilionyesha umati wa Wahindu wanaodaiwa kuwanyanyasa wanafunzi waliokuwa wakiandamana.

Wanafunzi hao waliokuwa wakiandamana walikuwa wamewasilisha maombi katika Mahakama Kuu ya Karnataka kupinga kupigwa marufuku kwa hijabu vyuoni.

Video iliyowekwa kwenye mtandao wa Twitter ikimuonyesha mwanafunzi Muislamu aliyevaa hijabu akibughudhiwa kwa maneno na genge la Wahindu wenye misimamo ya kufurutu mpaka katika chuo kimoja cha jimbo la Karnataka nchini India, imezusha moto wa hasira na kuzidisha malalamiko ya kupinga marufuku ya uvaaji hijabu iliyowekwa katika taasisi za elimu za jimbo hilo.

Marufuku ya kuvaa hijabu iliyowekwa katika vyuo vya jimbo la Karnataka imeamsha wimbi la hasira za wanafunzi Waislamu, ambao wanasema, hiyo ni hujuma inayolenga imani yao ambayo inatambuliwa rasmi na katiba ya India, huku makundi ya Kihindu ya mrengo wa kulia yakitumia mabavu kuwazuia mabanati wa KiislAmu wasiingie vyuoni na hivyo kuibua mivutano ya kijamii jimboni humo.

3477769

Kishikizo: india waislamu pogba hijabu
captcha