IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Nukta za kuzingatia wakati wa kusoma Qur'an katikta Mwezi wa Ramadhani

15:33 - March 29, 2023
Habari ID: 3476777
TEHRAN (IQNA) - Mwezi mtukufu wa Ramadhani, unaosifiwa kuwa ni mwezi wa Qur'ani Tukufu, ni fursa nzuri zaidi ya kujikurubisha na kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na kutafakari aya zake.

Wale wanaosoma Qur'ani wanapendekezwa kuzingatia baadhi ya nukta muhimu ili wapate manufaa na malipo zaidi kutokana na amali zao njema. Kitabu cha "Kanz al-Maram fi Amal Shahr al-Siyam" kimebainisha baadhi ya nukta hizo.

  1. Usafi

Mtume Muhammad (SAW) aliwapendekeza Waislamu kupiga mswaki kabla ya kusoma Qur'ani Tukufu.

Wakati huo huo, Imam Ali (AS) aliwataka watu wasisome Quran bila ya kuwa na wudhu (udhu).

  1. Kuketi kuelekea Ka’aba

Inapendekezwa kwamba watu wakae kuelekea Ka’aba tukufu huku wakisoma Qur'ani Tukufu au dua.

  1. Mwombe Mwenyezi Mungu akulinde na Shetani maluuni

Aya ya 98 ya Surah An-Nahl inasema: “Na ukisoma Qur'ani mwombe Mwenyezi Mungu akulinde na Shetani maluuni.

Watu walimuuliza Imamu Sadiq (AS) jinsi gani mtu anapaswa kutafuta hifadhi kwa Mwenyezi Mungu. Imamu akasema: “Sema: ‘Najikinga kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye kusikia Mwenye kujua, kutokana na madhara ya Shetani.

  1. Tarteel

Neno "tarteel" limetajwa katika aya ya 4 ya Surah Al-Muzzammil. Akifasiri aya hiyo, Mtume Muhammad (SAW) alisema mtu asome Qur'ani Tukufu kwa kutafakari na asisome aya kwa ajili ya kuzimaliza tu.

Imam Sadiq (AS) alibainisha kuwa tarteel maana yake ni kusoma Qur'ani Tukufu kwa tafakuri na sauti nzuri.

  1. Kujizuia kuzungumza

Waislamu wanashauriwa kutozungumza katikati ya usomaji wa Qur'ani Tukufu au dua, isipokuwa inapobidi.

  1. Kutafakari kwa kina

Qur’ani Tukufu imesisitiza ulazima wa kutafakari kwa kina juu ya aya hizi: “Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.. (Surah Sad, aya ya 29)

  “Je! Hawaizingatii hii Qur'ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli? ( aya ya 24 ya Surah Muhammad.

Katika Khutba ya 193 ya Nahj al-Balagha, Imam Ali anawaelezea watu wema kama hivi: “Wakikutana na Aya inayoleta shauku (ya Pepo) wanaifuata kwa shauku, na roho zao huielekea kwa shauku, na wanahisi kama pepo iko mbele yao. Na wanapokutana na Aya iliyo na khofu (ya Jahannam) hutega masikio ya nyoyo zao kwa hiyo, na wanahisi kana kwamba sauti ya Jahannam na vilio vyake vinafika masikioni mwao.

  1. Kutekeleza mafundisho ya Qur'ani

Thawabu zote za kusoma, kuandika na kufundisha Qur’ani Tukufu zinalenga kuufahamu ukweli na kutekeleza dhana na mafundisho ya Qur’ani Tukufu.

  1. Kusoma Qur'ani Tukufu mara kwa mara

Katika sehemu ya wosia wake mrefu kwa mwanawe Muhammad Hanafiyyah, Imam Ali (AS) anasema: Iwe juu yako kusoma Qur'ani Tukufu, kutekeleza mafundisho yake, kuzingatia faradhi na maamrisho yake, kufuata yale yanayoruhusiwa na kuacha yale yaliyoharamishwa, kuzingatia maamrisho yake na makatazo yake, na kuisoma kila mchana na usiku, ... hivyo ni wajibu kwa kila Muislamu kutimiza ahadi hii kila siku, hata kwa kusoma Aya hamsini.

3482967

captcha