IQNA

Shiriki Mashindano ya 2 ya Qur'ani ya Thaqalayn TV katika Mwezi wa Ramadhani

20:19 - February 23, 2025
Habari ID: 3480258
IQNA – Televisheni ya satelaiti ya Al-Thaqalayn itafanya toleo la pili la mashindano ya usomaji wa Tarteel wa Qur’ani Tukufu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mashindano hayo yatafanyika kupitia Skype na yamepewa jina “Wa Rattil” (…na usome Quran kwa sauti tofauti - Aya ya 4 ya Surah Al-Muzzammil), mashindano hayo yataonyeshwa kila siku wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani .

Wale wanaotaka kushiriki katika tukio la Qur’ani wanapaswa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 40.

Washindani, ambao  kwa sasa ni wanaumu, wanatakiwa kuwasilisha faili la sauti lililorekodiwa la usomaji wao wa Tarteel wa moja ya kurasa zifuatazo za Qur’ani (60, 88, 125, 206 au 549) kwa Nambari ya Whatsapp ifuatayo: +9899999914320

Al-Thaqalayn ni kituo cha televisheni cha satelaiti kinachorusha vipindi mbalimbali vyenye mada za kidini na kitamaduni.

Televisheni hii ya lugha ya Kiarabu, ambayo ilizinduliwa katika Ramadan ya 2008, inalenga kukuza utamaduni wa Kiislamu na mafundisho ya Qur’ani Tukufu na Ahl-ul-Bayt (AS).

Inalenga pia kuimarisha taasisi ya familia ya Kiislamu kupitia vipindi maalum kwa wanawake, watoto na vijana.

3491983

captcha