IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Misri Kutuma wasomaji Qur'ani, wahubiri duniani kote Mwezi wa Ramadhani

18:01 - March 06, 2024
Habari ID: 3478459
IQNA - Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, Misri inapanga kutuma wasomaji Qur'ani na wahubiri katika nchi mbalimbali katika mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

Wizara ya Wakfu ya Misri imetangaza kuwa zaidi ya wasomaji Qur'ani yaani maqari na wahubiri 200 watatumwa katika nchi za Ulaya, Asia, Afrika, Amerika na Australia.

Taarifa hiyo imesema idadi ya waliotumwa kwa kila nchi itategmea ombi la nchi mwenyeji.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, maqari 23 na maimami wa Sala watakwenda Ujerumani, 23 Brazil, 16 Marekani, 11 Tanzania, 11 Venezuela, 10 Canada, 7 Australia, 6 Uingereza, na 7 Umoja wa Falme za Kiarabu, miongoni mwa wengine.

Maqari watashiriki katika vikao maalumu vya kusoma  Qur'ani katika nchi zinazowakaribisha huku wahubiri wakiongoza sala katika misikiti na mikusanyiko ya kidini wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mwezi wa Ramadhani (ambao huenda ikaanza Machi 12 mwaka huu) ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu.

Qur'ani Tukufu iliteremshwa kwenye moyo wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) katika mwezi huu.

Mwezi huu mtukufu ni kipindi cha kukithirisha sala, saumu, utoaji wa sadaka na uwajibikaji kwa Waislamu duniani kote.

Wakati wa Ramadhani, Waislamu hufunga (kujiepusha na vyakula na vinywaji na yote yaliyokatazwa) kuanzia wakati wa kabla ya Sala ya Afajiri hadi Magharibi.

3487448

Habari zinazohusiana
captcha