IQNA

Ukombozi wa Palestina

Wapalestina waadhimisha "Yaumul Ardh" au Siku ya Ardhi

16:00 - March 31, 2023
Habari ID: 3476788
TEHRAN (IQNA) – Wapalestina ndani na nje ya nchi yao siku ya Alhamisi waliadhimisha kumbukumbu ya miaka 47 ya Siku ya Ardhi.

Ikumbukwe kuwa, Miaka 47 iliyopita katika siku kama ya leo, maandamano makubwa ya "Yaumul Ardh" au Siku ya Ardhi yalifanyika huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Tarehe 30 Machi inajulikana Palestina inayokaliwa kwa mabavu kuwa ni Siku ya Ardhi; na watu wa ardhi hiyo wanaiadhimisha siku hiyo.

Kuainishwa siku hiyo kunahusiana na matukio yaliyojiri Palestina mwaka 1976; siku ambayo wazayuni maghasibu walipora na kuhodhi sehemu kubwa ya ardhi za Wapalestina. Katika kubainisha hisia na malalamiko yao dhidi ya unyang'anyi huo, wananchi wa Palestina waliandamana, lakini kadhaa miongoni mwa waliuawa shahidi na wengine wengi walijeruhiwa.

Mkataba wa Oslo 2 wa mwaka 1995 ulizigawa ardhi za Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan katika maeneo matatu, ambapo eneo Alif liliwekwa chini ya udhibiti kamili wa Wapalestina, eneo Baa likawekwa chini ya udhibiti wa kiusalama, kiraia na kiidara wa Wapalestina na eneo Jim chini ya udhibiti wa kiraia, kiidara na kiusalama wa utawala wa Kizayuni. Ifahamike kuwa asilimia 60 ya ardhi ya Ufukwe wa Magharibi imetengwa kwenye eneo hilo la Jim.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi Kuu ya Takwimu ya Palestina, hivi sasa utawala ghasibu wa Kizayuni unahodhi na kutumia zaidi ya asilimia 85 ya ardhi yote ya Palestina kulingana na mipaka ya kihistoria, inayojumuisha UIfukwe wa Magharibi, Ukanda wa Gaza na Israel.

3482995

 

captcha