IQNA

Jinai za Israel

Hamas yalaani kitendo cha utawala wa Kizayuni kuuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa

16:51 - March 26, 2023
Habari ID: 3476764
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amelaani vikali uvamizi wa wanajeshi wa Kizayuni katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji mtakatifu wa al-Quds (Jerusalem).

Abdul Latif al-Qanoua katika taarifa yake alisema utawala wa Kizayuni umevunjia heshima utukufu wa Msikiti wa Al-Aqsa na mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Amesema kushambulia eneo hilo takatifu na kuwaondoa Wapalestina waliofunga katika msikiti huo ni ongezeko la hatari na kwamba utawala unaokalia kwa mabavu unawajibika kwa matokeo yake.

Askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamevamia Msikiti wa Al-Aqsa na kuwatia nguvuni Wapalestina kadhaa waliokuwa kwenye Itikafu na ibada zingine za mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Msikiti wa Al-Aqsa, ikiwa ndio nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na Kipalestina katika mji wa Baitul Muqaddas daima umekuwa ukiandamwa na hujuma na vitendo vya uharibifu vya utawala ghasibu wa Kizayuni.

Madhumuni ya hujuma na uvamizi huo unaoendelea kila uchao ni kuandaa mazingira ya kutekeleza mpango mwovu wa kuugawanya msikiti mtukufu wa Al-Aqsa kimahali na kiwakati katika matumizi baina ya Waislamu na Mayahudi, ili hatimaye Wazayuni waweze kuudhibiti kikamilifu msikiti huo na kuchukua hatua zinazolenga kuuyahudisha na kuubomoa na kujenga kwenye magofu yake hekalu la uzushi la Kiyahudi.

Chini ya kivuli cha serikali ya Benjamin Netanyahu yenye misimamo mikali na ya kufurutu mpaka na kuwemo ndani ya serikali hiyo mawaziri wenye misimamo mikali kama Itamar Ben Gower, ambaye ni waziri wa usalama wa ndani, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni alfajiri ya kuamkia leo wamewashambulia na kuwatia nguvuni Wapalestina kadhaa waliokuwa ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa wakifanya Itikafu na ibada zingine za mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Utawala wa Kizayuni vilevile umezikamata simu za mikononi za wale waliotaka kurekodi picha za vitendo hivyo vilivyo kinyume cha sheria ili walimwengu wasipate kujua kuhusu vitendo vya kinyama vilivyofanywa na askari wa utawala huo katili.

Khatibu wa Msikiti wa Al-Aqsa, Shekhe Ikrima Sabri, amesema kuhusiana na hatua hiyo ya kishenzi ya wazayuni kwamba utawala ghasibu wa Kizayuni umeanzisha kampeni yake ya kiwendawazimu dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa, kwa kupigana vita na wanaomwabudu Mwenyezi Mungu ndani ya msikiti huo kuwahamisha wafanya Itikafu.

4129921

captcha