IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa Mashindano ya Qur’ani ya Al-Kawthar TV watangazwa, Qari wa Afghanistan aibuka mshindi

18:30 - April 21, 2023
Habari ID: 3476898
TEHRAN (IQNA)-Washindi wa toleo la 16 la Mashindano ya Kimataifa ya Quran ya Televisheni ya Al-Kawthar TV wametangazwa jana usiku ambapo Qari wa Afghanistan ameibuka mshindi..

Morteza Nassar Ahmad Rahmani alipata nafasi ya kwanza katika mashindano hayo huku Muhamed Attieh kutoka Iraqi, Mojtaba Harandizadeh kutoka Iran, Saad Mohyeddin kutoka Lebanon, na Muhamed Ebrahim Muhamed Esmail kutoka Misri wakichukua nafasi zilizofuata kwa utaratibu huo.

Fainali ya mashindano hayo ilifanyika Alhamisi usiku.

Mashindano hayo ya Qur'ani Tukufu yanayofanyika kwa njia ya simu yamepewa anuani ya "Inna lil-Muttaqina Mafaza" (Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu- Quran Tukufu, Surat An Nabaa  aya ya 31) hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Jumla ya wahifadhi Qur’ani 36 kutoka nchi tofauti kama Iran, Iraqi, Afghanistan, Pakistan, India, Indonesia, Moroko, Algeria, Misri, na Lebanon walishiriki mwaka huu.

Ni mashindano makubwa zaidi ya ulimwengu ya Kiislamu ya usomaji wa Qur'ani moja kwa moja kwa njia ya televisheni yanayorushwa na Al-Kawthar, Televisheni ya lugha ya Kiarabu ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB).

4135744

captcha