IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Jisajili Mashindano ya 18 ya Qur'ani Tukufu ya Al-Kawthar TV

17:06 - January 13, 2025
Habari ID: 3480048
IQNA – Kituo cha Televisheni cha Al-Kawthar kimetoa mwaliko wa kushiriki katika toleo la 18 la mashindano yake ya Qur'ani kwa njia ya televisheni yaliyopangwa kufanyika katika mwezi wa Ramadhani 2025.

Kulingana na kituo hicho, usajili wa tukio hilo utaanza 13 Rajab 1446 sawa na Januari 14, 2025, sambamba na maadhimisho ya kuzaliwa kwa Imam Ali (AS), na utafungwa Februari 2, 2025, siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Imam Hussein (AS).

Mashindano hayo ya Qur'ani Tukufu yanayofanyika kwa njia ya simu yamepewa anuani ya "Inna lil-Muttaqina Mafaza" (Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu- Quran Tukufu, Surat An Nabaa  aya ya 31) hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Washiriki wanaotarajiwa wanaweza kujisajili kupitia tovuti rasmi ya mashindano (https://mafazatv.ir/register/)  au kuwasiliana na waandaaji kupitia WhatsApp au Telegram kwa namba +989108994025.

Washindani wanahitajika kuchagua na kusoma kwa sauti sehemu ya dakika mbili hadi tatu kutoka kwenye moja ya sehemu tatu za Qur'ani Tukufu: aya za 161–165 za Surah Al-An’am, aya za 143–144 za Surah Al-A’raf, au aya za 110–115 za Surah Hud.

Kurekodiwa kwa sauti pamoja na jina kamili la mshiriki, nchi, namba ya simu, na kifungu cha aya kilichochaguliwa lazima kiwasilishwe kwa mchakato wa awali wa uchunguzi.

Washiriki tisini na sita (96) watachaguliwa katika hatua ya tathmini ya awali kabla ya Ramadhani.

Washindani watakuwa na siku tatu kuwasilisha video zao kwa ajili ya tathmini ya moja kwa moja na jopo la kimataifa la majaji.

Kutoka kwenye kundi hili, wasomaji 24 wataendelea kwenye nusu fainali, huku msomaji mmoja wa ziada akichaguliwa kwa kura za watazamaji. Fainali kubwa, ikijumuisha washiriki watano wa mwisho kutoka nchi tano tofauti, itafanyika usiku wa Eid al-Fitr ambapo washindi wa juu watatangazwa.

Qari wa Kiirani Hemmat Qassemi alishinda toleo la 2024 la mashindano haya.

Mashindano ni miongoni mwa makubwa zaidi ya ulimwengu ya Kiislamu ya usomaji wa Qur'ani moja kwa moja kwa njia ya televisheni na yanarushwa Al-Kawthar TV, Televisheni ya lugha ya Kiarabu ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB).

3491444

Habari zinazohusiana
captcha