IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya 17 ya Qur'ani ya Televisheni ya Al-Kawthar yafika nusu fainali

16:14 - April 07, 2024
Habari ID: 3478646
IQNA – Maqari waliofanikiwa kuingia katika awamu ya nusu fainali ya Mashindano ya 17 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Al-Kawthar TV wametangazwa.

Kulingana na Al-Kawthar TV, waliofuzu nusu fainali ni wale ambao wamepata alama za juu zaidi katika duru iliyopita.

Waliofanikiwa kuingia nusu fainali wanatoka nchi tisa, ambazo ni Iraq, Iran, Afghanistan, Misri, Lebanon, Algeria, Morocco, Bangladesh na Indonesia.

Duru ya nusu fainali ya shindano hilo ilianza Ijumaa jioni. Hatimaye, washiriki watano bora kutoka nchi tano tofauti wataingia kwenye fainali kuu, iliyoratibiwa mkesha wa siku kuu ya Idd  ul Fitr.

Mashindano hayo ya Qur'ani Tukufu yanayofanyika kwa njia ya mawasiliano ya intaneti yamepewa anuani ya "Inna lil-Muttaqina Mafaza" (Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu- Quran Tukufu, Surat An Nabaa  aya ya 31)  na hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ni mashindano makubwa zaidi ya ulimwengu ya Kiislamu ya usomaji wa Qur'ani moja kwa moja kwa njia ya televisheni yanayorushwa na Al-Kawthar, Televisheni ya lugha ya Kiarabu ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB).

3487830

Habari zinazohusiana
captcha