IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Mashindano ya 16 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Al-Kawthar TV yaanza

22:10 - March 22, 2023
Habari ID: 3476742
TEHRAN (IQNA) – Duru ya 16 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Kanali ya Televisheni ya Al-Kawthar yameanza leo Jumatano jioni.

Jumla ya wasomaji 36 wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi mbalimbali kama vile Iran, Iraq, Afghanistan, Pakistan, India, Indonesia, Morocco, Algeria, Misri na Lebanon watachuana kuwania nafasi ya kwanza.

Usajili wa shindano hilo ulianza Februari sanjari na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Ali (AS), Imam wa kwanza wa Shia na kuhitimishwa Machi 8, sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe ujio wake).

Waombaji waliwasilisha faili iliyorekodiwa ya usomaji wao wa aya za 161 hadi 165 za Surah Al-An’am, au aya 142 hadi 144 za Surah Al-A’raf, au aya 110 hadi 115 za Surah Hud.

Visomo vilivyowasilishwa vilichambuliwa na jopo la wataalamu wa Qur'ani na washindani 36 waliofanya vizuri zaidi walichaguliwa kushindania tuzo ya juu zaidi.

Kati yao, 24 watafuzu kwa nusu fainali na hatimaye qaris 5 bora watachuana katika raundi ya mwisho usiku wa kabla ya idul-Fitr.

Mashindano hayo ya Qur'ani Tukufu yanayofanyika kwa njia ya simu yamepewa anuani ya "Inna lil-Muttaqina Mafaza" (Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu- Quran Tukufu, Surat AnNabaa  aya ya 31) hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ni mashindano makubwa zaidi ya ulimwengu ya Kiislamu ya usomaji wa Qur'ani moja kwa moja kwa njia ya televisheni yanayorushwa na Al-Kawthar, Televisheni ya lugha ya Kiarabu ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wale wanaopenda wanaweza kutazama shindano kwenye Al-Kawthar TV au kupitia tovuti ya https://www.alkawthartv.ir/live

 

4129364

captcha