IQNA

Wanamichezo Waislamu

Mwanamieleka Mwislamu Sami Zayn atekeleza ibada ya Umra + Video

17:12 - May 28, 2023
Habari ID: 3477061
TEHRAN (IQNA) – Sami Zayn, mwanamieleka wa kulipwa wa Kanada mwenye asili ya Syria, ametimiza ndoto yake ya kutekeleza ibada ya Hija ndogo ya Umra huko Makka, mji mtakatifu zaidi katika Uislamu ulioko Saudi Arabia.

Mwanamieleka huyo ambaye jina lake halisi ni Rami Sebei, alisambaza picha akiwa ndani ya Msikiti Mkuu wa Makka, ambapo alikamilisha taratibu za ibada ya Umra

Sami Zayn ni mmoja wa wanamieleka wengi wa WWE ambao wako kwenye ziara  Saudi Arabia, ambapo tukio la Usiku wa Mabingwa 2023 liliandaliwa.

Sami Zayn ambaye ni muumini mwenye kufungamana na mafunzi ya dini ya Kiislamu alitoa shukurani na furaha yake kwa kuweza kufanya Umra, ambayo ni Hija ndogo ya hiari Makka ambayo inaweza kufanywa wakati wowote wa mwaka, tofauti na Hija, ambayo ni ibada ya lazima ambayo hufanyika katika kipindi maalum katika Mwezi wa Dhul Hija.

Alisema kuwa kufanya Umra ni mojawapo ya uzoefu bora zaidi wa maisha yake na kwamba atatunza faida za ibada hiyo milele.

Nje ya mieleka, Sami Zayn anajulikana kwa uanaharakati wake na kazi ya kibinadamu. Ameripotiwa kuhusika katika masuala mbalimbali ya kijamii na kisiasa, kama vile kusaidia wakimbizi wa Syria na kutetea haki za binadamu za Wapalestina. Pia anaendesha shirika lisilo la faida liitwalo Sami for Syria, ambalo hutoa msaada wa matibabu kwa watu nchini Syria.

4144053

captcha