IQNA

Qiraa ya Qur'ani

Kijana Mmisri mwenye uwezo wa ajabu wa kuiga usomaji Qur’ani wa maqarii maarufu duniani +Video

18:20 - June 04, 2023
Habari ID: 3477099
TEHRAN (IQNA) – Nureddin Ibrahim ni kijana wa Misri ambaye anajulikana kwa uwezo wake wa ajabu kuiga mitindo ya usomaji wa Qur’ani ya maqarii maarufu duniani.

Usomaji Qur’ani Tukufu wa kijana huyu mwenye umri wa 20 umewavutia mamilioni katika mitandao ya kijamii

Nureddin, ambaye ni mhitimu wa Kitivo cha Ufundi cha Chuo Kikuu cha Al-Azhar, amehifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu

Anasema anaweza kuiga visomo vya wasomaji 15 mashuhuri, akiwemo Sheikh Abdul Basit Abdul Samad na Sheikh Khalil al-Husari.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Qur'ani zimeenea kote katika nchi hii  ambayo imeweza kuibua wasomaji Qur’ani(maqarii) bora zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu.

4144992

captcha