IQNA

Harakati za Qur'ani

Qari wa Nigeria anayesoma Qur'ani Tukufu kwa kwa Mtindo wa Sheikh Abdul Basit (+Video)

17:41 - May 08, 2024
Habari ID: 3478789
IQNA - Usomaji wa hivi karibuni wa qari wa Tarteel wa Qur'ani kwa mtindo wa Sheikh Abdul Basit Abdul Samad umeibua sifa.

Khalid Ibrahim Thani, ambaye anatoka Nigeria, ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar cha Misri.

Qiraa yake yenye mvuto ilijiri  wakati wa hafla iliyofanywa na Jumuiya ya Msaada ya Abul Ainaian na Jumuiya ya Kimataifa ya Al-Azhar Alumni kuwaenzi washindi wa shindano la kimataifa la Qur'ani Tukufu lililofanywa na chuo hicho, el-Balad iliripoti.

Alisoma Aya za 9-15 za Surah Al-Isra wakati wa hafla hiyo:

Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa.

Na mwanaadamu huomba shari kama vile aombavyo kheri, kwani mwanaadamu ni mwenye pupa.

Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili. Tena tukaifuta ishara ya usiku, na tukaifanya ishara ya mchana ni yenye mwangaza ili mtafute fadhila itokayo kwa Mola wenu Mlezi, na mpate kujua idadi ya miaka na hisabu. Na kila kitu tumekifafanua waziwazi.

Na kila mtu tumemfungia a'mali yake shingoni mwake. Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu atakacho kikuta kiwazi kimekunjuliwa.

Ataambiwa: Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosha leo kukuhisabu.

Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume."

4214161

Habari zinazohusiana
captcha