IQNA

Waislamu Ulimwengu wa Magharibi

Mwelimishaji wa Kiislamu nchini New Zealand Apokea Tuzo

15:01 - June 07, 2023
Habari ID: 3477113
Tuzo ya Heshima ya Mfalme nchini New Zealand mwaka huu imekabidhiwa Maysoon Salama, mwalimu wa Kiislamu, mwandishi, na kiongozi wa jamii, kwa huduma zake za elimu na jamii ya Kiislamu.

Mwalimu huyo wa Kiislamu alisema amepokea tuzo hiyo kwa  unyenyekevu kupata heshima hiyo, Stuff iliripoti.

Sikutarajia na ninashukuru sana, inafurahisha sana  na inatia moyo sana, Salama alisema.

Lakini familia yangu haikushangaa, na wametuunga mkono sana.

Salama alikuja New Zealand na mume wake  na familia miaka 30 iliyopita. Alizaliwa Palestina na kukulia Kuwait, alimaliza elimu yake ya udaktari nchini Marekani kabla ya kuhamia Christchurch katika miaka ya 1990.

Akiwa amevaa hijabu yake, alikandamiza mawazo ya awali ya kuwa mgeni kwa jamii, na kuanzisha Jumuiya ya Kitaifa ya Udada wa Kiislamu mnamo mwaka  2000. Pia alifanya kazi kama mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Kiislamu la New Zealand kutoka mwaka  2012 hadi mwaka 2020.

Pia alianzisha na kuendesha shule za awali zisizo za faida za An-Nur huko Christchurch na Dunedin, shule za awali za Kiislamu za New Zealand.

Sikuzote nimependa elimu, ni nyenzo muhimu kwa mafanikio. Tunafuata mitaala ya Serikali, pamoja na kuongeza kitu cha Kiislamu. Tuna watoto wa rangi zote na  kutoka tabaka mbalimbali za maisha.

Mtoto wa Salama Ata Mohammad Ata Elayyan alikuwa miongoni mwa waliouawa katika mashambulizi ya kigaidi ya mwezi  Machi 15.

Baada ya matukio ya kutisha huko Christchurch mnamo mwaka 2019 mwezi Machi,  Salama alipendekeza mfululizo wa vitabu vya hadithi vilivyoundwa ili kusaidia na kusherehekea jumuiya ya Kiislamu ya New Zealand.

Christchurch ni mji mkubwa katika Kisiwa cha Kusini cha New Zealand na makao ya Mkoa wa Canterbury. Pia ni nyumbani kwa wakaazi wapatao  404,500, na kuifanya kuwa jiji la tatu lenye watu wengi zaidi New Zealand nyuma ya Auckland na Wellington.

 

3483834

Kishikizo: uislamu mwanamke Heshima
captcha