IQNA

Waislamu Marekani

Mwanamke Muislamu ni Mwenyekiti Mwenza wa kupambana na chuki New York

19:21 - January 24, 2024
Habari ID: 3478245
IQNA – Uteuzi wa Diwani Shahana Hanif, mwanamke Muislamu, kama mwenyekiti mwenza wa Kikosi Kazi cha kupambana na chuki cha Jiji la New York umepongezwa.

Tawi la  New York la Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu (CAIR-NY), shirika kubwa zaidi la kutetea haki za Waislamu wa Marekani, Jumatatu ilipongeza hatua hiyo.

Shahana Hanif, mwanamke wa kwanza wa mwenye asili Bangladesh na Muislamu kuchaguliwa katika Baraza la Jiji, atasimamia jopo la wanachama sita na mwenyekiti mwenza Eric Dinowitz.

Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa CAIR-NY Afaf Nasher alisema:

"Tunampongeza Diwani Shahana Hanif kwa kuwa mwanamke wa kwanza wa Kiislamu kuwa mwenyekiti mwenza wa Kikosi Kazi cha Baraza la Jiji la Kupambana na Chuki. Kama mwanamke wa Kiislamu, yuko katika nafasi ya kipekee ya kupambana vitendon vya chuki katika jamii nyingi zilizotengwa.

3486924

captcha