IQNA

Mwanamke Mmisri ahifadhi Qur’an nzima akiwa na miaka 80

20:32 - November 19, 2025
Habari ID: 3481541
IQNA – Mwanamke kutoka mji wa Qena, Misri, ameweza kuhifadhi Qur’an Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 80, licha ya kutokuwa na elimu ya kusoma na kuandika.

Fatima Atitou alifikia mafanikio haya baada ya juhudi za miaka 15 za kujifunza kusoma na kuhifadhi Qur’an Tukufu.

Katika usiku wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ambapo ametimiza miaka 80, baada ya kuushinda ujinga wa kutojua kusoma na kuandika, ameweza kuhifadhi Qur’an nzima , safari iliyojaa changamoto na azma thabiti.

Mafanikio haya ya Qur’an yalitangazwa katika hafla iliyoandaliwa na Chama cha Vizazi Vijavyo mjini Qena, ambapo waliokuwapo walimsaidia katika njia ya elimu na kuhifadhi Qur’an.

Katika hafla hiyo, Fatima Atitou pamoja na walimu na wasaidizi wake katika safari ya kielimu na kidini walienziwa

Kuhifadhi Qur’an yote katika umri huu ni ujumbe kwa kila mtu kwamba mradi kuna nia, umri si kizuizi cha kujifunza na kubadilika kwa maisha bora.

Ahmed Abdel Qader, mwenyekiti wa baraza la utawala wa Chama cha Vizazi Vijavyo, alisema: Fatima Atitou ana miaka 80 na hakuwa akijua kusoma wala kuandika; lakini kwa kuhudhuria madarasa ya kuondoa ujinga katika chama hiki, alijifunza kusoma na kuandika kwa muda mfupi, kisha akashiriki katika vikao vya kuhifadhi Qur’an na kanuni za Tajwid.

Akaongeza: Katika kipindi cha miaka 15, walimu mashuhuri akiwemo Sheikh Ismail Muhammad, Shaima Rajab, na Fatima Mahmoud walimfundisha Qur’an Tukufu. Na kwa heshima hiyo, hafla maalum iliandaliwa kumenzi yeye na walimu wake.

Qur’an Tukufu ndiyo Kitabu pekee cha dini kinachohifadhiwa kwa moyo na wafuasi wake. Tangu siku ya kwanza ilipoteremshwa, idadi isiyo na kikomo ya waumini katika kila jamii ya Kiislamu wamehifadhi Qur’an.

Qur’an ina Juzuu 30, Surah 114 na Aya 6,236.

4317667

Habari zinazohusiana
captcha