Quran Tukufu inaangazia miujiza ya Nabii Issa (AS), ambayo ilikusudiwa kuwasaidia watu kuamini.
Nabii Isa (AS) alikuwa na miujiza mingi ambayo ilikuwa ni dalili za utume wake na uhusiano wake na Mwenyezi Mungu ili watu wasadikike kwamba hakika yeye ni nabii wa Mwenyezi Mungu.
Muujiza wa kwanza wa Nabii Isaa ulikuwa kuzaliwa kwake, Kwa mujibu wa Quran Tukufu Bi Maryam (SA) alibeba mimba bila ya kuolewa au kuwa na mahusiano yoyote na mwanamume, Kwa mujibu wa Quran Tukufu kuzaliwa kwake kwa njia hii ilikuwa ni ishara kwa watu na rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Akasema; Hili ni kweli lakini Mola wenu Mlezi anasema; Ni mepesi sana kwangu tumeamua kukupa mtoto awe ni ushahidi wa kuwepo kwetu kwa wanadamu na rehema kutoka kwetu, Hili ni agizo lililokwisha wekwa, Tafsiri ya Aya ya 21 ya Surati Maryam.
Muujiza wa pili wa ulikuwa kuzungumza katika utoto yani akiwa mtoto Akasema mtoto; ‘Mimi ni mfuasi wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amenipa Kitabu na amenifanya Nabii, Tafsiri ya Aya ya 30 ya Surati Maryam.
Pia alikuwa na miujiza wakati wa utume wake wa kinabii, Kwa mfano, Tafsiri ya aya ya 49 ya Surati Al Imran inaashiria miujiza yake minne, nayo ni kutengeneza ndege halisi kwa udongo, kumponya kipofu aliyezaliwa kipofu, kufufua wafu, na kuwaambia watu juu ya yale yaliyofichika, Atakuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa Wana wa Israili ambaye atawaambia.
Nimekuleteeni muujiza kutoka kwa Mola wenu Mlezi, Mimi ninaweza kukuumbieni udongo katika umbo la ndege, Nikipuliza ndani yake, huwa atakuwa ndege wa kweli, kwa idhini ya Mungu,Naweza kuwaponya vipofu na wenye ukoma na kuwafufua wafu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, naweza kuwaambia mnachokula na mnachoweka akiba katika nyumba zenu. Huu ni muujiza kwenu kama mnataka kuwa na imani.
Muujiza mwingine wa Nabii Issa ulikuwa ni kumwomba mwenyezi Mungu ateremshie chakula kutoka mbinguni, Wanafunzi waliposema, ‘Ewe (Nabii) Issa, mtoto wa Maryamu, je, Mola wako anaweza kututeremshia meza kutoka mbinguni? Tafsiri ya Aya ya 112 ya Surati Al-Maidah.
Mwenyezi Mungu kasema; ‘Mimi ninakuleteeni, lakini yeyote miongoni mwenu akigeuka na kuwa makafiri, nitamtia adhabu ambayo hajawahi kuipata yeyote Tafsiri ya Aya ya 115 ya Surati Al-Ma’idah.