IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Msichana wa Kenya ashinda Mashindano ya Qur'an Tukufu nchini Marekani

16:04 - July 12, 2023
Habari ID: 3477272
MINNESOTA (IQNA) - Msichana Mkenya mwenye umri wa miaka 17 alishinda tuzo ya kifahari ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Marekani.

Muna Abdifarah alitawazwa katika hafla ya kupendeza iliyofanyika baada ya kuwashinda washindani wake katika Mashindano ya 2 ya Kila Mwaka ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tibyan ya Marekani ambayo yalifanyika Minnesota.

Msichana huyo wa kidato cha pili anatoka  Shule ya Kiislamu ya Musa’b katika mtaa wa Eastleigh, Nairobi. Tukio hilo liliandaliwa na Kituo cha Sayansi cha Tybian. "Mabrouk (hongera) kwa mshindi wetu wa kwanza wa kitengo cha wanawake: Muna Abdifarah," kituo kilisema baada ya kumtangaza msichana wa Kenya kuwa mshindi wa shindano hilo.

Mshindi wa kwanza wa kitengo cha wanaume alikuwa Omar Afouf kutoka Ufaransa. "Hongera kwa washindi wetu, na shukrani za dhati kwa washiriki wote, majaji, na jumuiya yetu inayotuunga mkono," kituo hicho kilisema.

Abdifarah aliandamana na mwalimu wake, ambaye pia ni mkurugenzi Shule ya Kiislamu ya Musa’b,  Jama Wardere na mwanazuoni wa kimataifa wa Qur'ani Abdirashid Ali Sufi.

Mwaka jana, Aabdifarah alimaliza katika nafasi ya tatu duniani, katika shindano hilo.

Shule ya Kiislamu ya Musa’b kilianzishwa mwaka 1999. Tangu kuanzishwa kwake, kimekuwa kikishiriki katika mashindano ya Qur'ani yanayofanyika ndani na nje ya nchi ambapo kiliorodheshwa kuwa Madarasa bora katika mashindano hayo. Shule hiyo iliorodheshwa ya kwanza na ya tatu katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yaliyofanyika Rwanda na Dubai mtawalia.

Mnamo 2012, Shule ya Kiislamu ya Musa’b iilianzisha mfumo jumuishi wa masomo ya Kiislamu na pia masomo ya kiakademia ya mfumo wa elimu wa Kenya. Shule ya Kiislamu ya Musa’b imepanga kuchangisha pesa mnamo Julai 23, na Waziri wa Ulinzi wa Kenya Aden Duale ndiye atakaye kuwa mgeni mkuu wa hafla hiyo.

3484308

captcha