IQNA

23:07 - April 14, 2019
News ID: 3471916
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 36 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yamemalizika leo nchini Iran kwa kutangazwa washindi ambapo mwanafunzi kutoka Kenya ni miongoni mwa washindi.

Washindi waliotunukiwa zawadi ni wale walioshiriki katika mashindano ya kawaida ya wanaume, mashindano maalumu kwa ajili ya wanawake, mashindano ya wanafunzi wa shule na mashindano ya walemavu wa macho.

Mshiriki  kutoka bara la Afrika aliyepata nafasi bora zaidi katika mashindano ya mwaka huu alikuwa ni Abdulalim Abdulrahim Mohammad Haji ambaye alishika nafasi ya kwanza  katika mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani ya wanafunzi wa shule kitengo cha wavulana

Washindi wa mashindano hayo walikuwa ni wafuatao kwa utaratibu.

Mashindano ya Qiraa ya Qur'ani ya Wanaume

1 Salman Amrullah wa Indonesia

2 Mahdi Gholamnejad wa Iran

3 Mohammad Salman wa Iraq

4 Ahmad Amirabdulaziz wa Misri

5 Wan Ainuddin wa Malaysia

Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Wanaume

1 Mohammad Jawad Muradi wa Iran

2 Abdile Tawfiq wa Algeria

3 Ahmad Badruddin Hamami wa Syria

4 Ahmad Osama wa Mauritania

5 Akram bin Zakari Al Baqluti wa Tunisia

Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Wanawake

1 Maryam Shafii wa Iran

2 Fatima Yunis wa Lebanon

3 Samane Musavi wa Afghanistan

Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Wanaume Wenye Ulemavu wa Macho

1 Al Sayyid Hamdi Al Sayyid Ibrahim wa Misri

2 Said Ali Akbari wa Iran

3 Sayyid Nurul Haq wa India

Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Wasichana Wanafunzi wa Shule

1 Zainab Aminpour wa Iran

2 Faizah Nargiss wa Uturuki

3 Rim Ashbul wa Jordan

Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Wavulana Wanafunzi wa Shule

1 Abdulalim Abdulrahim Haji wa Kenya

2 Ali Faidhi wa Iran

3 Mahmoud Abulkheir Nasif wa Syria

Mashidano ya Qiraa ya Qur'ani ya Wavulana wa  Shule

1 Amir Hussein Rahmati wa Iran

2 Sayyid Yasin Husseini wa Afghanistan

3 Moahmmad Rafqi Hawari wa Indonesia

Washiriki 184 wa mashindano ya Qur'ani kutoka nchi 84 walifanikiwa kufika katika nusu fainali ya mashindano ya mwaka huu.
Nusu fainali ya mashindano hayo ilifanyika Jumanne Aprili 9 na Jumatano Aprili 10 asubuhi kabla ya ufunguzi rasmi wa fainali alasiri ya Jumatano ambapo mashindano yamemalizika Aprili 14.

Washindi wametunukiwa zawadi katika sherehe ambazo zimefanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA hapa Tehran ambao pia ulikuwa mwenyeji wa mashindano ya wanaume huku ya wanawake yakiwa yamefanyika katika ukumbi mwingine maalumu.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano ya kimataifa ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani ya Iran kila mwaka na huwa na washiriki kutoka kila kona ya dunia.

3803638

Name:
Email:
* Comment: