Watoto wenye umri wa miaka 4 walishiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi na kusoma sehemu za Qur'ani Tukufu.
Mashindano yam waka huu yalionyesha juhudi za mshiriki mmoja mwenye umri wa miaka 9 anayeitwa Maryam Bianouni. Bianouni alikuwa mshindi wa pamoja wa kwanza katika tukio hilo. Mafanikio yake yalikaribishwa kwa shangwe.
Bianouni ana hali nadra inayoharibu ukuaji na uwezo wa kuzungumza. Bianouni amejifunza jinsi ya kuwasiliana kwa msaada wa mama yake, Samia Mubarak, kwa kuandika kupitia iPad. Hiyo ni njia moja aliyoitumia kujiandaa kwa mashindano.
“Nilkuwa namfundisha baadhi ya aya kabla ya kulala. Ilikuwa kama sehemu ya utaratibu wetu wa usiku kwa wiki chache zilizopita,” alisema Mubarak. "Na jinsi tulivyomsaidia ni kwamba kila aya — tuliikata karibu kama kipande cha fumbo. Hivyo wakati alikuwa tayari, tuliweka vipande vyote 25 mbele yake. Kisha aliweza kuviweka vyote kwa mpangilio peke yake.”
Mashindano hayo yalimpa Bianouni fursa ya kuungana na jamii.
“Nataka apate nafasi katika jamii na kujua kwamba tunampenda kama watoto wengine wote wanaosoma. Na anaweza kufanya mambo kwa njia yake mwenyewe, na bado kusherehekewa kwa kiwango sawa.”
Mubarak anasema anatumai juhudi za binti yake zitaongeza motisha kwa wengine katika siku zijazo kushiriki katika mashindano ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
3492501