IQNA

Umrah 1445

Saudia yatoa maelezo kwa wale wanaotaka Visa ya Umrah

17:50 - July 20, 2023
Habari ID: 3477313
MAKKA (IQNA) – Wizara ya Hijja na Umrah ya Saudia imeeleza machaguo mbalimbali wka Waislamu wanaotaka kusafiri hadi mji mtakatifu wa Makka kufanya ibada ya Hija ndogo ya Umrah. Wizara iliorodhesha machaguo kama kama vile visa ya kukaa kwa muda mfupi (transit), visa ya kutembelea familia, visa ya safari ya kibinafsi na visa wakati wa kuwasili.

Wizara hiyo iliorodhesha machaguo kama kama vile visa ya kukaa kwa muda mfupi (transit), visa ya kutembelea familia, visa ya safari ya  kibinafsi na visa wakati wa kuwasili.

VISA YA KUTEMBELEA FAMILIA

Walei walio na visa ya kutembelea familia wanaweza kufanya Umrah lakini wanahitaji kuhakikisha kuwa wameweka miadi au kujisajili kupitia aplikesheni au tovuti ya  Nusuk.

Wanaweza kupata visa ya kutembelea familia kupitia jamaa anayeishi katika Ufalme wa Saudia.

Hadhi ya mwanafamilia inapaswa Raia/Mkazi.

Mahujaji wanaweza kutuma maombi kupitia tovuti jumuishi ya kitaifa ya Wizara ya Mambo ya Nje kwenye https://visa.mofa.gov.sa

 

VISA YA ZIARA BINAFSI

Raia wa Saudia wanaweza kualika marafiki zao kwenye Ufalme kufanya Umrah kwenye visa ya kibinafsi ya kutembelea nchi.

Faida ya visa ya kibinafsi ni kwamba ni visa ya chaguo moja au nyingi ya kuingia. Wanaowasilisha ombi wanaweza kufanya ibada za Umrah na kutembelea Msikiti wa Mtume SAW jijini Madina..

Wanaweza pia kutembelea maeneo ya kihistoria na maeneo mengine ya kitamaduni katika miji mbalimbali ya Ufalme wa Saudia.

Wanaweza pia kufanya safari za kitalii kwa mikoa na miji yote ya Saudi Arabia.

Visa moja ya kuingia inadumu kwa siku 90 na unaweza kukaa katika Ufalme kwa muda wa siku 90.

Visa ya kuingia na kutoka mara kadhaa pina inadumu kwa muda wa  siku 90.

Wanaotaka visa hii wanaweza kutuma maombi kupitia tovuti ya  visa ya Wizara ya Mambo ya Nje kwenye https://visa.mofa.gov.sa

 

VISA YA KUKAA KWA MUDA MFUPI (Transit)

Wanotaka kutekeleza ibada ya Umrah wanaweza kutumia visa ya kukaa kwa muda mfupi ikiwa tu wanawasili kwa ndege. Miongoni mwa faida za visa hii  ni kwamba wanaweza sio tu kufanya ibada ya Umrah bali pia kutembelea Msikiti wa Mtume SAW. Visa hii nayo pia inaweza kudumu kwa siku 90 baada ya kuipata na ukiingia Saudia unaruhusiwa kukaa kwa muda wa siku nne tu kwa siku nne. Visa hii haina malipo  na hutolewa mara unaponunua tikiti ya ndege.

Wanaotaka kutekeleza Ibada ya Umrah wanaweza kuchukua tikiti na kutuma ombi la visa kupitia majukwaa ya kielektroniki ya Saudia Airlines au Flynas.

Visa hutolewa kufuatia utoaji wa tikiti za ndege kupitia tovuti jumuishi ya kitaifa ya Wizara ya Mambo ya Kigeni.

 

VISA WAKATI WA KUWASILI

Raia wa Uingereza, nchi za Umoja wa Ulaya, Marekani na Kanada katika eneo la Amerika ya Kaskazini, Australia na New Zealand katika ene la eneo la Oceania, na halikadhalika raia wa Japan, China Singapore, Korea Kusini, Brunei, Malaysia na Kazakhstan wanaweza kuwasilisha maombi ya visa wakati wa kuwasili Saudia.

Masharti ya visa ni umri mwenye kujitegemea kwa ajili ya Umrah haupasw kuwa chini ya miaka 18; Muda wa kumalizika pasipoti usiwe chini ya miezi sita; Msafiri ni sharti apate  bima ya matibabu iliyoidhinishwa ndani ya Ufalme. Ada ya Visa itatozwa kwa mujibu wa maelezo.

Kishikizo: umrah 1445 saudia visa
captcha