IQNA

Umra 1445

Waislamu milioni 10 wanatarajiwa kushiriki katika Hija ndogo ya Umrah Msimu Huu

13:51 - July 09, 2023
Habari ID: 3477256
MAKKA (IQNA) - Waislamu milioni 10 kutoka nje ya Saudi Arabia wanatarajiwa kushiriki katika Hija ndogo ijulikanayo kama Umrah, makadirio yanaonyesha.

Televisheni ya Al Arabiya ya Saudia imesema kuwa ufalme huo unajiandaa kwa msimu mkubwa wa Umrah na unalenga kupokea Waislamu milioni 10 kutoka nje ya nchi ili kutekeleza ibada ya Umra katika Msikiti Mkuu wa Makka kuanzia Muharram, mwezi wa kwanza katika kalenda ya mwezi ya Kiislamu ambayo unatarajiwa kuanza chini ya siku 10 zijazo.

Takriban kampuni 300 zinazotoa huduma za Umrah zimetuma maombi na kupata leseni zinazohusiana, ripoti hiyo iliongeza.

Wiki iliyopita, Wizara ya Hija na Umrah ya Saudia ilisema imeanza kutoa visa za kielektroniki kwa ajili ya msimu mpya wa Umra baada ya kumalizika kwa ibada ya Hija ya kila mwaka.

Wizara ilisema maombi ya kupata visa ya Umrah yanawasilishwa kupitia tovuti ya Nusuk https://www.nusuk.sa/ar/about

Wenye viza wataanza kuwasili katika ufalme huo kufanya Umra kuanzia siku ya kwanza ya Muharram.

Jukwaa la Nusuk linawezesha taratibu ikiwa ni pamoja na malazi kwa Waislamu kutoka duniani kote wanaopanga kufanya Umrah.

Mamilioni ya Waislamu, ambao hawawezi kumudu ibada za kila mwaka za Hija kimwili au kifedha, wanamiminika Saudi Arabia kufanya Umra.

Katika miezi ya hivi karibuni, ufalme huo umezindua vifaa vingi kwa Waislamu wa ng'ambo kuja nchini kufanya Umra.

Waislamu walio na aina tofauti za visa vya kuingia kama vile za kibinafsi, za kutembelea na za kitalii wanaruhusiwa kufanya Umra na kutembelea Al Rawda Al Sharifa, lilipo kaburi la Mtume Muhammad (SAW) kwenye Msikiti wa Mtume wa Madina baada kujisajili kupitia tovuti.

Mamlaka ya Saudia imeongeza muda wa visa ya Umrah kutoka siku 30 hadi 90 na kuruhusu wamiliki kuingia katika ufalme huo kupitia njia zote za ardhini, anga na baharini na kuondoka kutoka uwanja wowote wa ndege.

Ufalme huo pia umetangaza kwamba walio na visa za  Schengen, Marekani na Uingereza wanaweza kujisajili kwa ajili ya Umrah na kutembelea Al Rawda Al Sharifa, kupitia programu ya Nusuk kabla ya kuwasili Saudi Arabia.

captcha