Tabia hizi mbili za kimaadili humsaidia mtu kufikia uongofu katika ulimwengu huu na ujao, ni funguo za kugundua Undani wa watu (ubinafsi wa ndani) Kwa hiyo ikiwa unataka kujua kuhusu tabia nzuri na mbaya za mtu, unapaswa kuzijaribu kwa ukweli na uaminifu.
Tabia hizi mbili zina athari nyingi nzuri katika maisha ya mtu, Kwa mfano wao husaidia kuongeza ufahari na heshima ya mtu miongoni mwa watu wengine, Ndio maana Imam Ali (AS) alihimiza kila mtu kuwa mkweli daima, kwa sababu mtu ambaye ni mkweli katika maneno yake, hadhi yake itakua katika jamii.
Ukweli pia humpa mtu ujasiri na ushujaa ambao kwa huo anaweza kupata amani ya akili, Uongo na unafiki, kwa upande mwingine, humfanya mtu kuwa na wasiwasi na woga kila wakati ili uwongo wake ufichuliwe na kupoteza heshima yake miongoni mwa watu.
Ukweli pia humfanya mtu kuwa thabiti katika kupinga madhambi na maovu, Kwa maneno mengine, inamsaidia kuepuka dhambi, anajua kuwa akifanya dhambi hawezi kuifunika, kwa hiyo anaepuka uovu na dhambi ili asije akajikuta katika hali hiyo.
Jinsi ya Kupata Baraka Zaidi za Mwenyezi Mungu
Ukweli na uwongo hudhihirika si kwa maneno tu bali pia kwa vitendo,wale ambao vitendo vyao ni kinyume cha wanavyohisi na kudhania ni waongo, Ndio maana wanafiki walipokwenda kwa Mtume Muhammad (S.A.W) na kushuhudia utume wake, iliteremshwa aya ya Qur’ani Tukufu ambayo ndani yake Mwenyezi Mungu anasema wanafiki wanasema uwongo, Muhammad (S.A.W) alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na huu ndio ukweli lakini wanafiki wanaposhuhudia haya, wanasema uwongo kwa sababu sivyo wanavyoamini moyon mwao.
Ukweli ni wa thamani sana mbele ya Mwenyezi Mungu kiasi kwamba anasema katika Tafsiri Aya ya 24 ya Surati Al-Ahzab; Hakika Mwenyezi Mungu atawalipa wakweli kwa ukweli wao na atawaadhibu au kuwasamehe wanaafiki apendavyo, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.