IQNA

Khums katika Uislamu/3

Angazio la Aya ya Qur’ani kuhusu Khums

21:02 - October 24, 2023
Habari ID: 3477781
TEHRAN (IQNA) – Uchumi ambao Uislamu unaupendelea ni ule uliochanganyika na maadili na hisia, na kuangalia aya kuhusu Khums ndani ya Qur’ani Tukufu kunadhihirisha vipengele muhimu vya suala hili.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 41 ya Surat Al-Anfal:

“Na jueni ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu na tuliyo yateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipo kutana majeshi mawili. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.”

Aya hii, kwa mujibu wa baadhi ya wafasiri wa Qur'ani Tukufu, iliteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW) wakati wa Vita vya Banu Qaynuqa (mwezi wa Shawwal mwaka wa pili baada ya Hijra) na wengine wanasema iliteremka wakati wa Vita vya Uhud (Shawwal ya tatu. Mwaka wa Hijri) au Vita vya Badr (Ramadhan ya mwaka wa pili wa Hijri). Mwenyezi Mungu katika Aya hii anawaita wale wanaopigan katika njia yake watoe moja ya tano ya waliyoyapata katika vita.

Kuna mambo muhimu katika aya hii, ikiwa ni pamoja na yafuatayo:

1- Kuna msisitizo mkubwa juu ya khums.

2- Aya inasema “Ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu” maana yake ni kwamba kulipa Khums ni sharti la kuwa na imani.

3- Ibara ya “Na jueni kwamba moja ya tano ya chochote mnachochukua ni cha Mwenyezi Mungu…” inaonyesha kwamba kanuni ni ya kudumu si ya muda.

4- Ibara ya “Wa A’alamu” (Na jueni) inaonyesha kwamba kulipa Khums lazima iwe ni imani na mtu lazima azingatie. Ifahamike kwamba kushiriki katika vita, kupigana pamoja na Mtukufu Mtume (SAW), kusali, kufunga, kuwa na imani, na kulishinda jeshi la adui haitoshi, kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema, "Ikiwa una imani, toa Khums". Ina maana kwamba hata ukifanya mambo yote hayo, unakosa imani ya kweli usipolipa Khums.

Imepokewa kwamba Mtukufu Mtume (SAW) hakulala usiku wa kuamkia vita vya Badr na alikuwa akiomba kila mara kwa ajili ya ushindi wa Waislamu, akisema hakuna kama watu hawa wachache hapa duniani na iwapo watashindwa, kuna hawatakuwa watu waaminifu tena. Lakini Qur’anI Tukufu inawahutubia watu hawa wachache sana na kusema kama wana imani, walipe Khums. Kwa maneno mengine, hata kundi hili dogo la watu ambao Mtukufu Mtume (SAW) anawaombea hawatahesabiwa kuwa ni waumini iwapo watashindwa kulipa Khums.

Kishikizo: khums qurani tukufu
captcha