IQNA

Zaka katika Uislamu /7

Faida za Kijamii za Zakat

13:58 - November 26, 2023
Habari ID: 3477950
TEHRAN (IQNA) – Kuna mamia ya Hadithi kuhusu kile kinachosaidia katika kuendeleza urafiki.

Zinaelekeza  kwenye mambo kama nia njema, tabia njema, ukarimu, sadaka, wema, hisani, n.k, yote hayo yanaweza kupatikana katika kulipa Zaka.

Hapa kuna faida za kijamii za kulipa Zakat:

Kuimarisha udugu

Qur'ani Tukufu inasema kuwa waumini ni ndugu (Aya ya 9 ya Surah Al-Hujurat). Pia inasema: “Wakitubu na wakasimamisha Salah na wakatoa Zaka, watakuwa ndugu zenu katika Dini. Basi tunazibainisha Aya zetu kwa watu wanao jua. (Aya ya 11 ya Surah At-Tawbah)

Kwa hivyo sharti la udugu ni kutoa Zaka, pamoja na toba na kuomba.

Kuondoa chuki

Kwa kutoa Zakat, chuki ya watu walionyimwa hugeuka kuwa wema na urafiki, ambayo itachangia kukuza ushirikiano na kusaidiana katika jamii na kulinda mafanikio ya jamii ya Kiislamu.

Kuwaondoa watu katika hali ya kutengwa

Umaskini na ufukara huwafanya watu kuwa kukata tamaa na kukosa tumaini na kujitenga. Lakini wakati Khums na Zakat zinapolipwa na matatizo ya kiuchumi ya watu yanatatuliwa nazo, furaha itaongezeka katika jamii na uwepo wa watu katika matukio ya kijamii utaongezeka.

Kukuza uelewa katika jamii

Kulipa Zaka huleta nyoyo karibu zaidi na kuandaa jamii kutatua matatizo. Ikiwa maskini wanajua wana sehemu katika faida ya matajiri, watakuwa na motisha ya kujitahidi kutatua matatizo ya jamii kadiri wawezavyo.

Kuondoa umaskini

Tatizo kubwa katika jamii zote ni kuwepo kwa umasikini, njaa na uhaba na njia mojawapo ya kukabiliana nazo ni kutilia maanani sana kulipa Khums na Zaka.

Kutengeneza ajira

Ukosefu wa ajira ni tatizo jingine muhimu katika jamii ambalo linaweza kusababisha matatizo mengine mengi. Iwapo watu watalipa Khums na Zaka kama wanavyotakiwa, uchumi utaanza kustawi na wengi wa wale ambao hawana kazi watapata kazi.

Kwa upande mwingine, kama watu wataacha kutoa Khums na Zaka na kuacha shughuli za kutoa misaada, kutakuwa na shinikizo kwa maskini, ambayo inaweza kugeuka kuwa machafuko katika jamii na ambayo yatadhuru kila mtu.

Kupunguza tabia mbaya za kijamii

Kujirundikia mali nyingi sana kunaweza kusababisha ufisadi lakini kulipa Khums na Zaka hutengeneza usawa na kuzuia ufisadi. Umasikini pia unaweza kusababisha ufisadi kwa njia ya wizi, kuchukua rushwa n.k. Maskini wanapopokea Khums na Zaka, misingi ya ufisadi huo huondolewa. Hivyo kulipa Khums na Zakat kuna nafasi muhimu katika kuzuia maovu ya kijamii.

Kulinda sifa ya maskini

Mara nyingi, umaskini unatishia sifa ya mtu. Kulipa Khums na Zaka huondoa umasikini na hivyo kulinda sifa za watu.

Kuondoa ukosefu wa mlingano katika mali

Khums na Zaka ni njia za kurekebisha mali. Uislamu unaweka njia wazi kwa wale wenye vipaji, wabunifu na kufanya kazi na kuwa matajiri. Pia inapiga marufuku mapato yanayopatikana kutokana na njia zisizofaa kama vile riba , wizi, hongo, ubadhirifu n.k. Kwa upande mwingine, Uislamu hauwaruhusu wale wanaopata pesa kwa njia za halali kutumia pesa zao kwa ubadhirifu na israfu. Uislamu pia umewajibisha Waislamu kutoa Khums, Zakat, Sadqat (sadaka), na kadhalika, ili kutatua matatizo ya watu wasiojiweza.

Kishikizo: qurani tukufu Zaka khums
captcha