IQNA

20:50 - November 25, 2023
Habari ID: 3477943
Umrah 1435

Ni wakati gani bora wa kutekeleza ibada ya Umrah katika Msikiti Mkuu wa Makka?

MAKKA (IQNA) – Afisa mwandamizi wa Saudia aliwapa ushauri Waislamu wanaolenga kutekeleza ibada ya Hija ndogo ya Umrah juu ya wakati gani ni mzuri wa ibada hiyo katika Msikiti Mkuu wa Makka au Masjid al-Haram.

Ni wakati gani bora wa kutekeleza ibada ya Umrah katika Msikiti Mkuu wa Makka?

Waziri wa Hija na Umra wa Saudia Tawfiq Al-Rabiah  amesema katika msimu huu muda  mzuri wa kuzuru Masjid al Haram kwa  ajili ya Umrah ni asubuhi ni kuanzia saa moja na nusu hadi saa nne na nusu na kisha usiku  kuanzia saa tano hadi saa nane.

Waziri huyo alisema katika taarifa yake kwenye akaunti yake ya X kwamba siku zisizo na watu wengi zaidi za kila wiki kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Umrah ni Jumapili, Jumanne, Jumatano.

Ushauri wa waziri huyo ulikuja wakati Msikiti Mkuu wa Makka ukishuhudia wimbi kubwa la waumini wanaotekeleza ibada ya Umrah wakitokea duniani kote.

Al-Rabiah alisema kuwa Makka imekuwa ikishuhudia hali ya hewa ya kupendeza siku hizi na hii inawawezesha waumini kutekeleza ibada zao kwa urahisi na utulivu wa kiroho.

Umrah  ni safari ya kwenda Makka ambayo Waislamu wanaweza kutekeleza wakati wowote wa mwaka, tofauti na Hija ambayo inaweza kufanywa tu katika siku za kwanza za mwezi wa Hijri wa Dhul Hajja.

3486148

captcha