IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Fainali za Mashindano ya 'Qari Bora Ulimwenguni' yamepangwa Aprili

17:25 - February 27, 2024
Habari ID: 3478422
IQNA - Duru ya mwisho ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa jina la "Qari Bora Duniani" itafanyika mwezi Aprili.

Wizara ya Wakfu  na masuala ya Kiislamu  Bahrain kila mwaka huandaa mashindano hayo ya Qur'ani.
Wasomaji na wahifadhi Qur'ani kutoka nchi 74 walishiriki katika hatua ya awali ya toleo la mwaka huu.
Kwa mujibu wa kamati ya maandalizi, jumla ya maqari na wahifadhi 5,092 walishindana katika awamu ya awali katika sehemu ya wanaume na wanawake.
Mwaka huu, kategoria ya kuhifadhi Qur'ani iliongezwa kwenye sehemu ya wanawake ya shindano hilo.
Jopo la wasuluhishi linalojumuisha wataalamu wakuu katika fani za sayansi ya Qur'ani, usomaji na Tajweed walitathmini  washindani na kuchagua walio bora zaidi kushindana katika fainali hizo.
Baada ya kumalizika kwa hatua za awali, kikao kilifanyika na kamati kujadili maandalizi ya fainali hizo na kuamua tarehe za mzunguko wa mwisho na kufunga.

3487349

captcha