IQNA

Vijana wahifadhi wa Qur’ani waenziwa nchini Bahrain

16:19 - April 23, 2025
Habari ID: 3480586
IQNA – Sherehe ilifanyika katika Mkoa wa Muharraq, Bahrain siku ya Jumatatu kwa ajili ya kuwaenzi vijana wa Bahrain kwa shughuli zao za Qur’ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Shaikh Mohammed bin Salman bin Hamad Al Khalifa alihudhuria sherehe hiyo na kueleza kuridhishwa kwake na dhamira ya serikali kuendelea kuwaunga mkono wahifadhi wa Qur’ani Tukufu.

Alisema kuwa Bahrain inatilia mkazo mkubwa katika kufundisha Qur’ani Tukufu na kuhamasisha kuihifadhi, juhudi ambazo zimeendelezwa kwa vizazi kadhaa.

Aliwaenzi vijana wa Bahrain wenye umri kati ya miaka 15 hadi 20 waliotoa mchango katika kuandaa swala za Taraweeh na Qiyam wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, pamoja na wale waliokamilisha kuhifadhi Qur’ani yote na kusambaza tilawa zao kupitia redio na televisheni za kitaifa.

Shaikh Mohammed alisisitiza kuwa ubora katika usomaji na uhifadhi wa Qur’ani ni chanzo cha fahari ya kitaifa na alitoa pongezi zake kwa waandaaji wa tukio hilo.

3492803

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu bahrain
captcha