Ayatullah Qassim amesema katika taarifa yake kwamba vikosi vya usalama vya Bahrain vinaendelea kuwazuia Waislamu wa madhehebu ya Shia kuswali Swala ya Ijumaa katika msikiti huo, gazeti la Manama Post limeripoti.
Ameitaja hatua hiyo kuwa vita vya kila wiki dhidi ya msikiti huo na dhidi ya kumwabudu Mwenyezi Mungu vinavyoendeshwa kwa ajili ya kumfurahisha Waziri Mkuu wa utawala wa Israel na Uzayuni khabithi.
Kila Ijumaa, vikosi vya usalama vya Bahrain hufunga mitaa inavyoelekea katika kitongoji cha Al-Diraz na kuzuia watu kwenda kwenye Msikiti wa Imam Sadiq (AS) kwa ajili ya Swala ya Ijumaa, alibainisha.
Wakati baadhi ya watu wanajaribu kwenda msikitini, wanakutana na risasi na mabomu ya machozi, aliongeza. Hivi ni vita ambapo uhuru wa watu wa kidini unakiukwa na hisia zao za kidini zinaumizwa, kasisi huyo alisema.
Hivi ni vita vya kila wiki ambavyo ni vya kikandamizaji, vya kijinga, vya kejeli na vya kipuuzi, na kuvielezea kuwa vimekataliwa kabisa na kulaaniwa. Hatua hii inalenga kuzuia kusikika kwa neno lolote kuhusu uungaji mkono wa Uislamu katika vita dhidi ya Wazayuni ambao wameanzisha vita vya kikatili (dhidi ya Ukanda wa Gaza) ambapo hakuna thamani wala sheria ya binadamu inayoheshimiwa, Ayatullah Qassim alisikitika.
3490714