IQNA

Ibada ya Hija Mazoezi ya Jihad: Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

7:50 - June 18, 2024
Habari ID: 3478972
IQNA - Hija ya mwaka huu ni Hija ya "mazoezi ya jihad" na fursa kwa mataifa ya Kiislamu kuachana na utawala haramu wa  Israel na waungaji mkono wake wakuu wa nchi za Marekani na Magharibi.

Haya ni kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kanaani, akitoa matamshi hayo katika mtandao wa X kupitia ukurasa wake siku ya Jumapili alisema, huku kukiwa na vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelea vya utawala ghasibu dhidi ya Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

N vile vile mamilioni ya mahujaji wa Kiislamu kutoka kote duniani wamekusanyika mjini Makka huko Saudi Arabia, kutekeleza ibada ya Hija ya kila mwaka.   

Falsafa ya Hija Nabii  Ibrahimu (as) na mila na desturi zake hufundisha Waislamu na waumini kila mahali duniani jinsi ya kutangaza kumkana Shetani na wale wenye tabia za kishetani katika ulimwengu halisi.

Afisa huyo aliendelea kusema kuwa, suala la bara'at (kuwakana washirikina) mwaka huu linapaswa kwenda zaidi ya ibada ya Hija na kuenea kwa mataifa yote ya Kiislamu duniani, kama alivyotangaza Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayid Ali Khamenei katika ujumbe wake wa kila mwaka wa Hija, alisema;

"Kujitoa kwa utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake hususan serikali ya Marekani ni lazima kudhihirike katika kauli na vitendo vya mataifa na serikali, na kunapaswa kukaza kamba kwa wanyongaji, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran, Nasser Kan'ani aliongeza kwa kusema.

Zaidi ya mahujaji milioni 1.5 kutoka sehemu mbalimbali za dunia tayari wamekusanyika ndani na nje ya Makka kwa ajili ya Hija, huku mahujaji zaidi kutoka ndani ya Saudi Arabia wakiendelea kujiunga na Mamlaka ya Saudia iliyotarajia jumla ya mahujaji mwaka huu kuzidi milioni 2.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi  ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Ali Khamenei Anasisitiza Kukanusha Utawala wa Kizayuni,  na waungaji mkono  wake wakuu Wamarekani na Wamagharibi. 

Ibada ya Hija ya mwaka huu inafanyika kutokana na vita vinavyoendelea vya mauaji ya halaiki ya Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa na kusababisha vifo vya takriban watu 37,337 wengi wao wakiwa wanawake na watoto na kujeruhi wengine zaidi ya 85,299.

Wapalestina kutoka Ukanda wa  Gaza hawakuweza kusafiri hadi Makka mwaka huu kutokana na kufungwa kwa kivuko cha Rafah mwezi Mei wakati utawala katili wa Israel ulipopanua uvamizi wake wa ardhini hadi Rafah, mji wa kusini kwenye mpaka wa Ukanda wa Gaza na Misri.

 

 

https://iqna.ir/en/news/3488783

 

 

captcha