Ayatollah Makrim Shirazi ni Marja maarufu mamlaka ya kidini, chanzo cha kuigwa kwake madhehebu ya Shia.
Kiongozi wa Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Sayid Ali Khamenei, alimtembelea katika hospitali moja huko mjini Tehran.
Katika ziara hiyo, Imam Khamenei aliuliza kuhusu maendeleo ya matibabu ya Ayatullah Makarim Shirazi na kumuombea apone haraka na awe na afya njema.
“Katika miaka hii yote, maisha yako yamebarikiwa na umekuwa na manufaa katika masuala ya ujuzi wako wa kisayansi, mwongozo wako kwa watu, na hekima yako.
Mwenyezi Mungu aendelee kukupa baraka zake,” aliongeza kwa kusema; Kiongozi wa Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Sayid Ali Khamenei,
Kwa upande wake, Ayatullah Makarim Shirazi, pia alitoa shukurani zake kwa wema na huruma ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.