Maombolezo ya Muharram, yaliyoandaliwa na Muslim Khoja Shia Ithna-Asheri (MSKI), yalirejea jijini kwa mara ya kwanza tangu 2019.
Muharram ni mwezi wa kwanza wa kalenda ya Kiislamu wakati Waislamu wa madhehebu ya Shia wanapoadhimisha ibada za kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na masahaba zake katika Vita vya Karbala vya mwaka 680 AD.
Msafara wa Leicester ulianzia Humberstone Gate, ukipitia East Gates, High Street kabla ya kuishia Jubilee Square, Mratibu wa maombolezo hayo ya muharram ni Ali Abbas Rajani, alisema Imam Hussein (AS) alikuwa mtu ambaye watu wanaweza "kupata msukumo kutoka kwake."
Ilikuwa ni kukataa kwake kuonyesha uaminifu kwa Yazid, kulikopelekea kuuawa kwake kishahidi. Msimamo wake pamoja na utetezi wake wa haki za binadamu ndizo sababu anazoadhimishwa ndani ya jumuiya ya Shia.
Ali Abbas alisema: “Maombolezo ya muharram ni ukumbusho tu, na Kueneza maadili yake na kuhamasisha wengine kurudisha nyuma kwa jamii kila wakati.
"Iwapo ni kusimama kwa haki za binadamu, kusimama dhidi ya dhuluma, kulisha maskini, kutunza wasio na makazi, kupenda na kulea yatima, kusaidia jirani au kueneza tu upendo na huruma. Tunaamini kwamba Imamu Hussein (AS) anaweza kuwa mtu ambaye unaweza kupata msukumo kutoka kwake.
"Iwapo kila mtu hivi sasa angefanya hata badiliko moja dogo la chanya katika maisha yake au mchango mdogo kwa jamii kwa sababu jambo fulani kutoka kwa maisha ya Imamu Husein (AS) lilimgusa moyo, basi tutalichukulia hilo kuwa ni mafanikio makubwa. Katika kila ardhi na wakati, kwa kila taifa na kabila, hadithi ya Imamu Husein (AS) inatoa msukumo na kutia moyo kwa watu: kufahamu dhulma na kuchukua hatua, hata kama ni ndogo, kuzungumza na kuchukua hatua dhidi yake.
Kituo cha Kiislamu cha Uingereza Huandaa Maombolezo ya Muharram kila mwaka
Huu ulikuwa mwaka wa 32 kwa maombolezo hayo kufanyika mjini Leicester, hata hivyo kitendo cha ukumbusho kimekuwa kikiendelea kwa zaidi ya karne 13 duniani kote.
3489151