IQNA

Kuuawa Shahidi Siyo Mwisho Bali Ni Mwanzo wa Kuamsha Mataifa

18:47 - July 05, 2025
Habari ID: 3480900
IQNA – Utamaduni wa Ashura hauangalii kufa shahidi kama mwisho wa safari bali ni mwanzo wa kuamsho wa mataifa, amesema mwanazuoni kutoka Iran.

Hujjatul Islam Abdollah Hassani, mkuu wa ofisi ya mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika vyuo vikuu vya mkoa wa Ardebil, alitoa kauli hii katika mahojiano na IQNA kabla ya siku ya Ashura, tarehe 10 ya Muharram, ambayo ni kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS).

Amesisitiza kuwa ushindi wa hivi karibuni wa Iran dhidi ya utawala wa Israel haukuwa tu mafanikio ya kijeshi bali ni dhihirisho la roho ya kudumu ya Ashura, inayohimiza mapambano kote katika ulimwengu wa Kiislamu.

Amehimiza umuhimu wa kufundisha vipengele vya kielimu, kiakili na vya tukio la Ashura kwa kizazi cha wasomi, na kuongeza kuwa: "Vyuo vikuu vinapaswa kuwa mstari wa mbele katika kukuza utamaduni wa uelimishaji, kuleta mwangaza na 'Jihadi ya Kufafanua Ukweli'."

 Akielezea ujumbe muhimu zaidi wa Ashura kwa vijana, alisema: “Ujumbe muhimu ni uwajibikaji wa kiakili mbele ya ukweli na uongo. Imam Hussein (AS) anatufundisha kutosalia kimya mbele ya ufisadi wa kimfumo, kupotoka kwa itikadi na dhulma ya kihistoria. Huu ni mwito wa daima wa kuamka, kuchukua hatua, na kufanya jihadi kwa ajili ya haki.”

Ameongeza kuwa wanafunzi wa leo wanapaswa kutambua kuwa jukumu lao halijazuiliwa tu kwa maendeleo ya kitaaluma bali pia ni kufufua haki, maadili, na umaanawi. Ashura ni mfano wa kuchanganya hisia, mantiki na azimio na ni mfano unaoweza kuwaokoa vijana kutoka katika hali ya kutokuwa na mwelekeo na uzembe.

Msomi hiyo amesema kuwa kusambaza mafundisho ya Imam Hussein (AS) katika mazingira ya vyuo vikuu kunahitaji mbinu za kina na za kipekee. Sifa kama kama vile heshima, ujasiri, ghera ya dini, uaminifu kwa ukweli na kujitolea nafsi zinapaswa kufikishwa kwa kizazi cha wasomi kupitia programu za kielimu, kiutamaduni na kisanii.

Martyrdom Not An End But Start of Path to Nations’ Awakening: Cleric

Aidha ameelezea umuhimu wa kujifunza kutokana na mifano ya kihistoria ya Ashura katika kujenga maadili kama hekima ya Habib ibn Mazahir, ushujaa wa Bibi Zainab (SA) na uaminifu wa Hadhrat Abbas (AS). Vyuo vikuu vinapaswa kuwa sehemu za kuendeleza haki, uwajibikaji wa kijamii, kupambana na ufisadi, na kulinda heshima ya mwanadamu na siyo tu mahali pa vyeti au hadhi za kijamii.

Amebainisha kuwa Ashura ni wazo linalojenga ustaarabu, akisema: “Wazo hili linaangazia misingi kama vile Tawhid (umoja wa Mungu), haki, uongozi kwa msingi wa uchamungu, demokrasia ya Kiislamu, kujitolea kwa jamii na kupinga dhulma. Ashura inatufundisha kusimama dhidi ya upotovu wa kiustaarabuka kama ule upotovu wa utawala wa Umawiyyah hata tukiwa wachache, mradi tu tuna imani isiyotetereka.”

3493718

captcha