Walioivunjia heshima Qur'ani Uswidi kufikishwa kizimbani
IQNA - Uswidi (Sweden) itawafikisha mahakamani wanaume wawili walioivunjia heshima Qur'ani Tukufu mara kadhaa wakati wa maandamano mwaka jana, waendesha mashtaka wa nchi hiyo ya Skandinavia wametangaza.
Walisema Jumatano kwamba watenda jinai Salwan Momika na Salwan Najem walifanya "makosa ya uchochezi dhidi ya kabila au kikundi cha kitaifa" mara nne tofauti.
Mashtaka hayo yalisema kuwa wawili hao waliinajisi Qur'an', ikiwa ni pamoja na kuichoma, huku wakitoa matamshi ya dharau kuhusu Waislamu, katika kisa kimoja nje ya msikiti katika mji mkuu, Stockholm.
Matukio ya kuvunjia heshima Qur'ani ya majira ya joto ya 2023 yalikasirisha Waislamu duniani kote, na kusababisha Sweden kuimarisha usalama huku uhusiano wake na nchi za Asia Magharibi ukivurugika.
"Watu wote wawili wanashitakiwa kwa matukio haya manne kutoa kauli na kuitendea Qur'ani kwa namna iliyokusudiwa kuonyesha dharau kwa Waislamu kwa sababu ya imani yao," Mwendesha Mashtaka Mkuu Anna Hankkio alisema katika taarifa yake.
"Kwa maoni yangu, matamshi na vitendo vya watu hawa viko chini ya vifungu vya uchochezi dhidi ya kabila au kikundi cha kitaifa, na ni muhimu kwamba suala hili lihukumiwe mahakamani," aliongeza.
Ushahidi dhidi ya wanaume hao upo hasa katika rekodi za video, Hankkio alisema.
Najem alisema hakuwa na makosa, wakili wake, Mark Safaryan, aliambia shirika la habari la Reuters.
Momika, mkimbizi Mkristo kutoka Iraq, amesema alitaka kuandamana dhidi ya Uislamu na ametaka pia Qur'ani Tukufu ikipgwe marufuku.
3489694