IQNA

Waislamu Uingereza

Hukumu yatolewa kuwa Shirika la Waislamu wa Uingereza si la 'itikadi kali'

17:31 - October 05, 2024
Habari ID: 3479541
IQNA - Shirika Huru la Viwango vya Waandishi wa Habari (IPSO) limeunga mkono malalamiko ya Jumuiya ya Waislamu wa Uingereza (MAB) dhidi ya gazeti la The Telegraph ambali lilidai kuwa jumuiya hiyo ni taasisi yenye "itikadi kali."

Uamuzi huo, uliotangazwa siku ya Alhamisi, ulifuatia uchunguzi wa miezi saba katika makala ya Machi ambayo ilidai kuwa etu kuwa Jumuiya ya Waislamu wa Uingereza ni taasisi ya watu wenye msimamo mkali.

"IPSO imeafiki malalamiko yetu dhidi ya The Telegraph kwa kututaja kwa uwongo kama shirika lenye msimamo mkali, baada ya Michael Gove kutumia vibaya fursa ya ubunge katika kueneza ufafanuzi usio sahihi na wa kisiasa wa itikadi kali," ilisema MAB katika chapisho kwenye X.

IPSO imetoa hukumu kwamba gazeti hilo lilikiuka Kanuni za Utendaji za Wahariri kwa “kukosa kujizuia kuchapisha habari zisizo sahihi” na “kwa kukosa kusahihisha makosa makubwa kwa upesi wa kutosha.”

Nakala hiyo, iliyoandikwa na mchambuzi wa mrengo wa kulia Nick Timothy, ilidai MAB ilikuwa "moja ya mashirika kadhaa yaliyotangazwa kuwa ya itikadi kali na Michael Gove Bungeni." Hata hivyo, Gove alikuwa ameeleza kuwa MAB iliibua wasiwasi kutokana na "mwelekeo wake wa Uislamu" na kwamba serikali ingetathmini kama inaweza kutajwa kuwa taasisi ya itikadi kali.

Kujibu malalamiko hayo, The Telegraph ilitoa masahihisho kwenye ukurasa wake wa marekebisho na ufafanuzi, ikihusisha kosa hilo na "makosa ya kibinadamu."

"Wakati marekebisho yanakaribishwa, tunahimiza vyombo vya habari kutafakari juu ya wajibu wao wa kuripoti ukweli na kuepuka kueneza uongo unaodhuru," alisema MAB.

Uamuzi huo unakuja katika wakati mgumu, huku vyombo vya habari vya Uingereza vikikabiliwa na shutuma za upendeleo wakati huu ambapo Israel inaendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza na Lebanon. Vyombo vya habari Uingereza vimekuwa vikupendelea utawala wa Kizayuni wa Israel huku vikipuuza jinai zinazotendwa na utawala huo.

 3490142

Kishikizo: waislamu uingereza
captcha