"Jaribio la Bill Clinton lisilo na uaminifu kuhalalisha mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya raia huko Gaza lilikuwa la matusi sawa na lile la chuki dhidi ya Uislamu," alisema Robert S. McCaw, Mkurugenzi wa Masuala ya Serikali katika Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR).
"Haikubaliki kabisa kuukejeli Uislamu na kudai kwa uwongo kwamba kila mwanamume, mwanamke na mtoto wa Kipalestina aliyeuawa na Israel alikuwa anatumika kama ngao ya binadamu," aliongeza katika taarifa ya Alhamisi, kama ilivyoripotiwa na tovuti ya kundi hilo.
"Hata Rais Biden alikiri miezi kadhaa iliyopita kwamba serikali ya Israel imehusika katika mashambulizi ya kiholela ya mabomu huko Gaza," alibainisha na kuongeza, "Viongozi mashuhuri kama Bill Clinton wanapaswa kuzingatia haki za binadamu za Wapalestina, bila kuhalalisha uhalifu wa kivita dhidi ya raia wa Palestina."
Akiwa Michigan, Clinton aliwakosoa Wapalestina na Waamerika-Waarabu wanaopinga Utawala wa Biden-Harris kutokana na kuunga mkono wa vita vya Israel dhidi ya Gaza, ambavyo vimesababisha mauaji ya Wapalestina wasiopungua 43,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kusababisha sehemu kubwa ya Gaza kuwa isiyoweza kukaliwa na watu.
Clinton alisema kuwa Rais Biden alikuwa akitimiza "wajibu" wake kwa serikali inayokalia kwa kutoa msaada wa kijeshi bila masharti.
3490509