IQNA

Chuki dhidi ya Waislamu

Muislamu apigwa risasi na Kujeruhiwa nje ya Msikiti huko Rhode Island, Marekani

16:35 - November 18, 2023
Habari ID: 3477907
WASHINTON, DC (IQNA) - Mwanamume aliyekuwa akiuza bidhaa zinazohusiana na imani ya Kiislamu nje ya msikiti huko Providence, Rhode Island, alipigwa risasi na kujeruhiwa Ijumaa asubuhi, kulingana na polisi wa eneo hilo.

Tukio hilo limesababisha kuongezeka kwa doria katika eneo hilo huku mamlaka ikitafuta mshukiwa sambamba na kubaini lengo lake.

Mkuu wa polisi Oscar Perez alisema kuwa ufyatuaji risasi ulifanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Rhode Island.

Shambulio hilo linakuja  huku kukiwa na hali ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu nchini Marekani kufuatia vita kati ya Wapalestina na utawala wa Israel.

Mwathiriwa, ambaye ni huswali katika msikiti huo, alikuwa katika meza ya kuuza "bidhaa za Kiislamu" alipopigwa risasi sehemu ya chini ya mwili wake.

Afisa aliyekuwa karibu alisikia milio ya risasi na akaelekea eneo la tukio mara moja. Mwathiriwa mwenye umri wa miaka 52 baadaye alisafirishwa hadi hospitali kwa matibabu ya majeraha yasiyo ya kutishia maisha.

Katika mahojiano na WPRI, Perez alielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo na kusisitiza kuwa polisi watakuwa wakilinda usalama katika eneo hilo ili kuhakikisha usalama wa kila mtu.

Habari zinazohusiana
captcha