Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Zimbabwe kiliandaa maonyesho hayo kwa ushirikiano na ubalozi wa Palestina katika nchi hiyo ya Kiafrika na Baraza la Mshikamano wa Palestina, Shirika la Iran na Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO) limeripoti.
Maonyesho hayo yalikuwa na lengo la kuangazia machungu na mateso ya Wapalestina na ukatili na vita vya mauaji ya halaiki vya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Picha hizo zilionyesha hospitali, zahanati, kambi na makazi ya wakimbizi huko Gaza ambayo hupigwa mabomu na utawala wa Kizayuni kila siku.
Maonyesho hayo yalizinduliwa katika hafla iliyohudhuriwa na Balozi wa Palestina Tamir al-Misri na pia Balozi wa Iran Abbas Navazani.
Katika hotuba yake, al-Misri ameitaka jumuiya ya kimataifa kusitisha mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina na kuwafungulia mashitaka maafisa wa Israel kwa uhalifu wa kivita.
Amebainisha kuwa, asilimia 97 ya miundombinu ya matibabu huko Gaza imeharibiwa na utawala wa Israel unachukua dawa zinazohitajika na Wapalestina waliojeruhiwa.
Ameongeza kuwa wengi wa waliouawa huko Gaza ni watoto.
Navazani pia alitoa hotuba, akisisitiza kwamba Iran itaendelea kuunga mkono vikosi vya kupigania ukombozi wa Palestina na Lebanon.
Amesikitishwa na undumilakuwili wa nchi za Magharibi kuhusu mauaji ya kimbari na ukiukaji wa haki za Wapalestina.
Mzungumzaji mwingine, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Zimbabwe Sheikh Hinri Balakazi alisisitiza kwamba Wapalestina wanapigania uhuru, utu na kuishi katika nchi yao mama.
Ameongeza kuwa maonyesho hayo yanalenga kufichua jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wapigania uhuru wa Palestina.
Rabsum Musafara kutoka Taasisi ya Marafiki wa Palestina ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuendelea kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na Lebanon katika mapambano yao dhidi ya utawala wa kibaguzi wa Israel.
3490525