Alihukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa kesi mbili za "uchochezi dhidi ya makabila".
Aliambia vyombo vya habari kuwa anakusudia kukata rufaa.
Mwendesha Mashtaka Adrien Combier-Hogg alisema kwa kiasi fulani ameridhishwa na hukumu hiyo: "Kuhusu suala la hatia, yaani, sehemu ambayo inabainishwa kama amefanya uhalifu na ni uhalifu wa aina gani ... majaji wamehukumu kwa mujibu shitaka langu kwa sehemu kubwa.”
Hata hivyo, hukumu ya kifungo cha miezi minne iliyotolewa na mahakama ni nusu tu ya kile Combier-Hogg aliomba.
Kesi hiyo inatokana na matukio mawili huko Malmö mnamo 2022 ambapo Paludan alichoma Quran hadharani na kutoa matamshi kuhusu Uislamu ambayo mahakama iliona kuwa inastahili "kuchochea chuki dhidi ya kundi la watu."
Mahakama ya wilaya iliamua kwamba mwanasiasa huyo alionyesha kutowaheshimu Waislamu na kwamba hatua zake haziwezi kusamehewa tu kama ukosoaji wa Uislamu au kama kazi ya kampeni ya kisiasa.
Mnamo Julai, serikali iliwasilisha pendekezo ambalo lingewapa mamlaka haki ya kuzuia udhihirisho unaoonekana "kuhatarisha usalama wa nchi" - ikiwa ni pamoja na uchomaji wa Qur'ani, ambayo kwa sasa inalindwa chini ya sheria za uhuru wa kuzungumza za Sweden.
Vitendo vya kuchoma Qur'ani vya Paludan na wanaharakati wengine nchini Uswidi mwaka jana vilisababisha maandamano ya ghasia nchini Uswidi na duniani kote.
3490660