IQNA

Kikao cha Kusoma Qur’ani chafanyika Khan Yunis, Gaza

17:58 - March 18, 2025
Habari ID: 3480395
IQNA – Mkusanyiko wa kwanza wa kusoma Qur’ani nzima tangu mwaka 2023 ulifanyika katika jiji la kusini mwa Gaza la Khan Yunis. 

Zaidi ya wasomaji 200 walikusanyika kuhitimisha Qur’ani Tukufu.

Walihudhuria tukio hilo kuadhimisha mila za kidini katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Wakati huo huo walionyesha uvumilivu wao licha ya matatizo yaliyosababishwa na vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala haramu wa Israel. 

Mashambulizi ya utawala wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza yaliyoanza Oktoba 7, 2023, yameua zaidi ya Wapalestina 48,600, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kuwajeruhi zaidi ya 100,000 wengine. 

Hata vita hivyo havikuwafanya Waganda kuacha Qur’ani, kwani wengi walipata matumaini na uvumilivu katika mafundisho ya Qur’ani Tukufu ndani ya kambi za wakimbizi. 

Katika madarasa ya muda, walimu wa kujitolea wameongoza masomo, wakitoa utulivu kwa watu katikati ya hali ya msukosuko."

3492429

captcha