IQNA

Ayatullah Javadi Amoli: Qur'ani Tukufu huwa na ujumbe mpya kwa kila zama

10:06 - May 08, 2025
Habari ID: 3480653
IQNA – Qur'ani Tukufu daima hubeba ujumbe mpya kwa kila kipindi, amesema mwanazuoni mwandamizi wa Kiislamu Ayatullah Abdollah Javadi Amoli.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akihutubia kongamano mjini Qum siku ya Jumatano, lililofanyika kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Kiislamu (Hauza) cha Qum na mwanzilishi wake Ayatullah Mkuu Haj Sheikh Abdulkarim Haeri Yazdi (RA).

Alimnukuu Imam Ali (AS) akisema katika Nahj al-Balagha kwamba kitabu ambacho hakina mfano ni Qur'ani. Ayatullah Javadi Amoli aliongeza kuwa wataalamu wa kweli wa Qur'ani na wafasiri wake ni Ahl-ul-Bayt (AS). Alisema Qur'ani Tukufu na Ahl-ul-Bayt (AS) ni misingi ya kuwaongoza watu wasipotee.

“Kwa hiyo, tunapaswa kujitahidi kunufaika na Qur'ani na Ahl-ul-Bayt (AS) ili tupate ucha Mungu na wokovu.”

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Javadi Amoli alisifu mafanikio makubwa ya marehemu Ayatullah Haeri Yazdi, yaani kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Qom.

Alisema alama kuu na sifa muhimu ya Ayatullah Haeri Yazdi, ambaye aliweza kufufua Qurani, elimu za akili, fiqhi, na misingi zaidi ya hapo awali, lazima zitafutwe.

Kongamano hilo la kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Qum lilihudhuriwa na idadi kubwa ya wanazuoni na viongozi wa chuo hicho.

Jumbe kutoka Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei na baadhi ya wanazuoni wakubwa kama Ayatullah Nasser Makarem Shirazi na Ayatullah Hossein Ali Nouri Hamedani zilisomwa katika kongamano hilo.

4280908

Kishikizo: qurani tukufu qum
captcha