IQNA

Mabadiliko katika mipango ya Hija baada ya kuandama mwezi wa Dhul Hijjah

15:36 - May 28, 2025
Habari ID: 3480755
QNA – Kufuatia tangazo la kuanza kwa mwezi wa Hijria wa Dhul Hijjah, serikali ya Saudi Arabia imepitia upya mipango ya msimu wa Hija wa mwaka huu katika kikao kilichofanyika Jumanne.

Mahakama Kuu ya Saudi Arabia imetangaza kwamba mwezi wa Dhul Hijjah utaanza siku ya Jumatano.

Hija hufanyika katika mwezi wa Dhul Hijjah, na Hija ya mwaka huu itaanza tarehe 4 Juni ambapo Mahujaji watakusanyika katika mji wa mahema wa Mina.

Baraza la Mawaziri la Saudi Arabia limesema kuwa taasisi husika zinafanya kazi kwa viwango vya juu zaidi vya ufanisi, ubora, uratibu, na mshikamano, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Saudi (SPA).

Jitihada hizi zinalenga kuhakikisha faraja na usalama wa Mahujaji, zikisaidiwa na miradi ya maendeleo na miundombinu ya kisasa, ambayo huboresha huduma zote na kurahisisha utekelezaji wa ibada za Hija kwa mahujaji kutoka kote duniani, limesema Baraza hilo.

Hija ni safari ya ibada kuelekea mji mtakatifu wa Makka ambayo kila Muislamu mwenye uwezo wa kimwili na kifedha analazimika kuitekeleza angalau mara moja katika maisha yake.

Hija ya kila mwaka inachukuliwa kuwa ni moja ya nguzo tano za Uislamu na ni ibada kubwa zaidi ya pamoja duniani. Pia ni ishara ya umoja wa Waislamu na utii wao kwa Mwenyezi Mungu.

3493250

Kishikizo: hija
captcha