IQNA

Nakala 15,000 za Qur’ani na vitabu vya Sala vyasambazwa katika kaburi la Hadhrat Abbas (AS) nchini Iraq

17:38 - July 19, 2025
Habari ID: 3480966
IQNA – Idara inayosimamia kaburi au Haram ya Hadhrat Abbas (AS) huko Karbala, Iraq imetangaza usambazaji wa takriban nakala 15,000 za Qur’ani Tukufu na vitabu vya sala kwa ajili ya matumizi ya mamilioni ya waumini wanaotembelea eneo hilo takatifu.

Idara hiyo mesema imeandaa takriban nakala 15,000 za Qur’ani Tukufu, vitabu vya ziyara, na dua mbalimbali kwa ajili ya mamilioni ya waumini wanaotembelea eneo hilo takatifu.
Sayyid Hussein Al-Mousavi, Misahafu hiyo na vitabu husambazwa hasa katika nyakati maalum kama Muharram,  Arbaeen, Idi ya Nisf Shaaban.

Kaburi la Hadhrat Abbas (AS) huko Karbala lipo karibu na kaburi tukufu la Imam Hussein (AS).
Maeneo haya mawili matakatifu huvutia mamilioni ya waumini kutoka sehemu mbalimbali za Iraq na duniani kote kila mwaka, hasa wakati wa miezi ya Hijri ya mwezi Muharram na Safar. Eneo baina ya haram hizo mbili tukufu hujulikana kama Bayn al-Haramayn. 

3493894

captcha